loader
Picha

Kituo Namanga kilete tija Tanzania, Kenya

MARAIS John Magufuli na Uhuru Kenyatta jana walifungua kituo cha utoaji huduma kwa pamoja Namanga mkoani Arusha, mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Kituo hicho kinatarajiwa kurahisisha huduma za forodha, uhamiaji, usalama wa raia na biashara kati ya wananchi wa nchi hizo mbili kutokana na huduma kuwa sehemu moja.

Tunaungana na Rais Magufuli na Rais Uhuru kuwapongeza wananchi wa Tanzania na Kenya, kwa kupata kituo hicho kitakachorahisisha zaidi mwingiliano na biashara kati yao mpakani.

Pia tunaungana na marais hao, kuipongeza Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na pia Shirika la Maendeleo la Japan (Jica) kwa misaada waliyotoa kufanikisha miradi husika.

Ni fahari kubwa kwa Tanzania na Kenya kupata kituo cha kisasa mpakani kama hicho, huku marais hao wakisema kingine kiko mbioni kujengwa Isebania mpakani mwa Kenya na Tanzania huko mkoani Mara na barabara ya kutoka Malindi hadi Bagamoyo mkoani Pwani.

Kufunguliwa kwa kituo hicho na vingine vitakavyokuja ni ushahidi wa jinsi wana Afrika Mashariki wenyewe, wanavyoweza kuendesha mambo yao na kuimarisha zaidi ushirikiano.

Ndio maana tunaungana na marais hao, kuwataka wananchi wa pande zote mbili kuishi kama ndugu, huku wakishirikiana kwa hali na mali kama jamii moja, licha ya kutenganishwa na mipaka iliyowekwa na wakoloni kwa ajili ya kurahisisha ajenda ya kuitawala Afrika.

Tunaomba kituo hiki kichochee maendeleo ya biashara kati ya nchi hizo mbili na hasa zile zinazohusu wanyonge na wajasiriamali, kama alivyosema Rais Uhuru kuwa ndio nguzo ya uchumi wa nchi kutokana na wingi wao, kinyume na wengi wanavyoamini ni wale wakubwa.

Ni matumaini yetu kuwa wafanyabiashara husika, watakaopitisha mizigo, bidhaa zao, huduma zao katika kituo hicho, watatumia fursa hiyo vizuri na si kuwa chanzo cha rushwa kwa watu au watumishi wanaohudumu katika kituo hicho, wakilenga kukwepa kulipa kodi ya serikali.

Wafanye hivyo wakijua lengo kuu la serikali hizo mbili kuboresha kituo hicho na kuweka pamoja huduma zote zinazohusu kuvuka mpakani, lilikuwa ni kuwarahisishia wafanyabiashara wakubwa na wadogo, uendeshaji wa biashara zao kwa lengo la kuzipatia kodi stahiki.

Si vyema basi kama kutakuwa na wafanyabiashara, watakaokitumia kituo hicho kwa maslahi binafsi, kinyume na matarajio ya serikali, badala ya kuimarisha mtangamano wa wananchi na zaidi uchumi wa zao ili hatimaye maendeleo zaidi yaweze kupatikana kwa pande zote mbili.

Tunaziomba taasisi husika kujipanga vyema kwa ajili ya kutoa huduma nzuri, zaidi ya vile zilikuwa zikifanya huko nyuma, kwani sasa mazingira ya kazi yameboreshwa zaidi, kuondoa vikwazo vyote vilivyokuwa kwa namna moja au nyingine, vikichangia kuchelewesha huduma zao.

HAKUNA ubishi kwamba ili kuimarisha biashara yoyote ile duniani, zikiwemo ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi