loader
Picha

Mradi wa maji Arumeru utunzwe

RAIS John Magufuli jana aliweka jiwe la msingi la mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 520 zilizotolewa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo yaAfrika (AfDB).

Tunaishukuru Benki ya AfDB kwa fedha hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zitasaidia kutatua shida ya maji katika wilaya Arumeru kwani mbali na kuokoa maisha ya wakazi hao, lakini pia imeongeza imani kwa wananchi wa wilaya hiyo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya maji.

Ndio maana Rais Magufuli wakati anaweka jiwe hilo la msingi akasema mradi huo wa maji utawasaidia wananchi wa maeneo hayo kupata maji safi na salama na akaagiza Mamlaka za maji kuwaunganishia maji wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji.

Tunaungana na Rais Maguguli kwamba Watanzania wanachotaka hivi sasa ni kuona fedha au miradi inayofanyika inawanufaisha.

Ni ukweli ulio wazi kwamba Mtanzania hataki maneno ya siasa ambayo yamejaa ushawishi lakini utekelezaji wake hakuna.

Tunaamini kuweka jiwe hilo la msingi ni mwanzo wa ukamilishaji wa mradi huo ambao wananchi wengi watapata maji yaliyo safi na salama.

Ni kutokana na ukweli huo, Rais Magufuli akamwagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa kuhakikisha wakandarasi waliopewa kazi za kukamilisha mradi huo mkubwa wa maji wanafanyakazi Tunaamini Benki ya AfDB itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa serikali yetu sikuvu ambayo imedhamiria kuwakomboa wananchi hasa wanyonge kila kona ya nchi.

Tumeipokea kwa mikono miwili rai aliyoitoa mwakilishi wa benki hiyo, Alex Mobiru kwamba mradi huo wa maji unaonesha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Akasisitiza kwamba mradi huo unaendana na malengo ya waanzilishi wa benki hiyo ili kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa na maendeleo ambapo utaboresha huduma mbalimbali za maji.

Kwa mtizamo wake, anasema hakuna mtoto atakayekosa kwenda shule sababu ya maji ikiwemo wananchi kuwa walemavu sababu ya kukosa maji.

Ni imani yetu kwamba wananchi wa Arumeru watakuwa tayari kushirikiana katika ulinzi wa mradi huo ili miundombinu yake isiharibiwe na watu wasiopenda maendeleo.

Watakuwa tayari kuilinda kwa nguvu zao zote ili kuendelea kufaidi matunda ya ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwsa), Ruth Koya ili kufanikisha mradi huo wa maji wana wakandarasi 10 waliojumuisha uchimbaji wa visima 11 vikiwemo vikubwa na vidogo.

Koya anasema mradi huo wa maji utanufaisha watu milioni moja wa kata saba za Wilaya ya Arumeru na mara baada ya mradi huo kukamilika, tatizo la maji litapungua na upungufu wa maji katika Jiji la Arusha utakuwa umekamilika.

Anasema kazi zilizopangwa ni kuchimba visima, kuongeza mtandao wa bomba za kusafirisha maji, ujenzi wa mabwawa wa kutibu maji na ujenzi wa vyoo vya mfano kwenye shule mbalimbali.

Anasema jumla ya visima 13 vimechimbwa ikiwemo ulazaji wa mabomba ya maji taka na ujenzi wa mabomba ya maji taka pia mradi huo wa utakapokamilika utawezesha wananchi wengine kupata maji na kupunguza wastani wa maji yanayopotea kufika asilimia 25.

HAKUNA ubishi kwamba ili kuimarisha biashara yoyote ile duniani, zikiwemo ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi