loader
Picha

Mtoto apata Benz kwa kupiga push-up 3000

Mtoto wa umri wa miaka mitano nchini Urusi amepata gari aina ya Mercedes Benz baada ya kushinda shindano la kupiga push-up 3200 kwa wakati mmoja.

Mtoto huyo Rakhim Kurayev  ambaye pia anafahamika kwa jina la 'Schwarzenegger wa miaka mitano' alipiga push-up hizo kwa muda wa saa 2 na dakika 22.

Kurayev anaripotiwa kuvunja rekodi sita za dunia za mchezo huo kwa nyakati tofauti. 

Amepewa gari hilo pamoja na mafasi ya kwenda duka lolote la ma-toy ya watoto na kuchukua chochote anachotaka.

Mmoja wa majaji wa shindano hilo Ramzan Kadyrov ameeleza kuwa Kurayev alifanya push-up 1000 kwa muda wa dakika 40 na sekunde 57, push-up 2000 kwa saa moja na sekunde 47 Pia alifanya nyingine 1419 kwa saa moja, huku 2559  akizifanya kwa saa mbili.

Mwanaume mkazi wa Bournemouth, Uingereza Laurence Vonderdell, 50, amehukumiwa kifungo ...

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi