loader
Miss Tanzania atikisa China

Miss Tanzania atikisa China

MWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya Dunia Queen Elizabeth Makune ameingia 15 bora ya warembo wanaopewa nafasi ya kushinda taji la ulimbwende kwa mwaka huu.

Shindano hilo la 68 la dunia limepangwa kufanyika Desemba nane jijini Sanya, China.

Katika taarifa ya mtandao wa GoPageant ambao huelezea na kuchambua mashindano mbalimbali ya urembo duniani, ulimtaja Queen Elizabeth ni mmoja wa warembo 15 kati ya 113 wanaoshiriki shindano hilo wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo lenye heshima duniani katika masuala ya urembo.

Mrembo huyo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), alitawazwa kuwa Miss Tanzania Septemba 8, mwaka huu na hii ni baada ya nyota yake kuanza kung’aa katika shindano la Miss Universe na baadaye Miss Dar es Salaam.

Mwandaaji wa Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi ameomba watanzania kuendelea kumpigia kura kwa wingi mshiriki huyo ili aweze kuipeperusha vema bendera ya Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya urembo duniani.

Basila ambaye ni Miss Tanzania mwaka 1998, aliwataka watanzania kumpigia kura mrembo huyo kupitia tovuti ya Miss World ya www.missworld.com.

Warembo wengine wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo ni Shrinkhala Khatiwada (Neval), Dayana Martinez (Puerto Rico) na Annukreethy Vas kutoka India.

Wengine ni Miss Chile, Anahi Hormazabal ambaye kama atashinda basi hii itakuwa ni mara ya pili kwa nchi hiyo kuondoka na taji hilo, Andrea Szarvas (Hungary), Maeva Coucke (Ufaransa), Agata Biernat (Poland), Morgane Theresine (Guadalupe), Solaris Barba (Panama), Elya Nurshabrina (Indonesia).

Pia yupo Taylah Cannon kutoka nchini Australia, Vanessa Ponce (Mexico) na Natalya Stroeva (Urusi).

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bb518d51973e9ae1a2564cdd9a393f87.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi