loader
Picha

MSD yaagizwa ijiendeshe kibiashara

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameitaka bodi ya wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) kuhakikisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinakuwa na ubora na bei nafuu kuliko hospitali na vituo vya huduma binafsi.

Amesema ikiwa watu binafsi wanafanya biashara ya dawa na kupata faida huku mitaji ikikua, vivyo hivyo bohari hiyo ijiendeshe kibiashara na fedha za dawa zinazouzwa katika vituo vya huduma zirudi ili kuongeza upatikanaji wa dawa nchini.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam, alipoizindua bodi hiyo ya MSD yenye wajumbe tisa ikiongozwa na mwenyekiti wake, Fatuma Mrisho; aliyekuwa Mwenyekiti Mtendandaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (Tacaids).

Alisisitiza bodi hiyo kuwa makini na ununuzi wa zaidi ya Sh bilioni 21 kwa mwezi unaofanywa na MSD kwa kusimamia mifumo na udhibiti ili kuondoa mianya ya upotevu wa fedha na ubadhirifu.

Alisema utendaji wa Mwenyekiti huyo wa bodi, unatosha kuwa na matumaini ya kuiongoza MSD katika mabadiliko ya kiutendaji na kuongeza nguvu katika kusimamia maboresho ya upatikanaji wa uhakika wa dawa na vifaa tiba.

"Aina ya bodi iliyopo nina amani na furaha, kasimamieni sheria, navitaka vituo vya afya , zahanati na hospitali za serikali kurejesha fedha za dawa wanazochukua serikalini, sitakuwa tayari na sitakubali kila siku kumuomba Rais John Magufuli Sh bilioni 270 halafu zisirudi au zikipatikana ziende kuboresha biashara za watu binafsi," amesema.

Amesema, vituo hivyo vimekuwa havirejeshi fedha za MSD kwa kisingizio cha kuwa na wagonjwa wengi wa msamaha huku akiwa na taarifa zaidi za ndani kuwa fedha hizo zinatumika kununua dawa katika vituo binafsi bila kufuata utaratibu, lengo likiwa ni asilimia 10 wanazoahidiwa na wafanyabiashara hao.

"Ni muhimu bodi hii kujua madhumuni na malengo ya uanzishwaji wa MSD na kuhakikisha wanaitumikia nchi kwa weledi na uzalendo, muhimu dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyopo katika bohari hiyo kuwa na ubora kuliko za huko nje," alisema.

Ummy alisema matarajio yake ni taasisi hiyo kujiendesha kibiashara huku ikizingatia ubora na gharama nafuu ili kila mwananchi aweze kujivunia huduma za afya zilizopo nchini.

"Nawahakikishia wale wanaofanya mchezo na fedha na dawa hizi za serikali, najua watu wanafungua kamradi huko pembeni wanachezesha nitawakamata tu," alisema.

Aliongeza kuwa ameanza mazungumzo na ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na wataalamu wa wizarani kwake kufanyia kazi changamoto zilizopo, kwa kuwa zamani kulikuwa hakuna fedha za dawa sasa zipo lakini imekuwa ni biashara isiyo na faida kwa kuwa hazirudi.

"Kisingizio kikubwa ni kuhudumia watu wa msamaha lakini hao watu ni asilimia 50 nirudishieni basi hata 50, dawa ni biashara kubwa sana na kwetu siyo biashara tu ni huduma na siasa tumetekeleza ilani fedha zipo hazionekani,” alisema.

Aliongeza, “Najua halmashauri wanaona ni zao, wanaenda kununu a huko sisi serikali si wakala wa kutafuta fedha ili mpeleke kwa wafanyabiashara bodi tushirikiane kwa kuwa wananchi wanauziwa hizi dawa."

Mwenyekiti wa bodi ya MSD, Mrisho aliahidi kufanya kazi kwa uwezo na weledi wote na kusema kwa kuwa maisha yake sehemu kubwa amehudumia jamii katika sekta ya afya akiwa ndani na nje ya nchi katika jumuiya za kimataifa atahakikisha anatumia uzoefu huo kwa maslahi ya taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Laurean Bwanakunu, alisisitiza haja ya mabadiliko ya sheri kuongeza uwezo wa kitendaji ndani ya bohari hiyo kwakuwa inapokuwa bodi haipo inampa wakati mgumu kuwa anawajibika kwa nani katika .

SERIKALI mkoani Songwe imewataka wakulima wa zao la alizeti kubadilika ...

foto
Mwandishi: Mariam Mziwanda, TurDACO

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi