loader
Picha

Aunty- Mwanangu mtamu kuliko chochote

MUIGIZAJI wa Bongo movie Aunty Ezekiel amesema yupo tayari kuzaa mtoto mwingine na mpenzi wake ambaye ni dansa wa WCB Mosses Iyobo.

Wawili hao tayari wana mtoto mmoja wa kike Cookie, ambapo kwenye mahojiano maalumu ametaja pia sababu za kumpa mwanaye jina hilo.

"Natamani sana, lakini bado kidogo, kuna vitu navikamilisha halafu ndiyo nifikirie kuzaa mtoto mwingine, siyo mmoja hata watatu kwa sababu mimi napenda sana watoto,”amesema Aunty.

Amesema sababu za kumpa mwanaye jina la Cookie ni kutokana na furaha aliyopata baada ya kuzaa.

"Unajua maana ya Cookie ni vibiskuti vile vidogo, lakini vitamu sana, sasa nilipomzaa tu niliona nimepata kitu kitamu sana kuliko chochote hapa duniani, nikaamua tu kumpa mtoto wangu jina hilo kumuonesha kwamba yeye kuwa mwanangu ni utamu tosha kwangu," amesema.

Katika kumuandalia mwanaye huyo maisha bora, Aunty amesema ametenga fedha nyingi kwa ajili ya kumsomesha mtoto wake ili kumtengenezea mazingira mazuri miaka ijayo.

YANGA imepania kushinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi