loader
Picha

Spika Eala aomba wakutane Zanzibar

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Martin Ngoga amesema, Bunge hilo ni taasisi inayotafakari na kuchukua hatua muafaka kwa mujibu wa matakwa ya nchi sita wanachama wa jumuiya kutekeleza majukumu iliyojipangia.

Ngoga ameyasema hayo alipozungumza na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Chukwani mjini Unguja.

Ngoga amefika Zanzibar kuomba ruhusa kufanya vikao vya Bunge hilo Zanzibar Februari mwakani.

Amesema zipo changamoto katika uwajibikaji wao.

Amesema wabunge wa Eala wamekuwa wakishiriki vyema vikao vya maamuzi yenye kuleta ustawi na mwelekeo unaozingatia hatma ya wananchi wake.  

''Nawapongeza kwa dhati wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa ushiriki wao vizuri katika Bunge hili ambao unatokana na maslahi ya nchi zao na wananchi,'' amesema.

Balozi Iddi amesema Bunge hilo likiwa na sauti moja katika maamuzi yake kwa kiasi kikubwa litaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo kwa faida ya nchi wanachama.

Alisema wananchi wa nchi za EAC matarajio yao makubwa baada ya kuundwa kwa jumuiya ni kuona mabadiliko ya kiuchumi sekta mbalimbali.

''Hayo ndiyo matarajio makubwa ya wananchi wa nchi za Afrika Mashariki....mabadiliko ya uchumi na maendeleo yanafikiwa kwa faida ya wengi”, amesema.

Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki kutoka Zanzibar, Makame Hasnuu amesema wakati umefika kwa Serikali za Afrika Mashariki kubadilisha mfumo wa Bunge litumie Kiswahili.

'’Kiswahili kinatumiwa na wananchi wote wa nchi sita za EAC na njia pekee ya kupata umaarufu zaidi ni Bunge kutumia lugha hiyo, '' amesema.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga ameonesha kukerwa na ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi