loader
Picha

Serikali yatafuta wabangua korosho

SERIKALI imeanza mchakato wa kupata wazabuni wa ndani na nje ya nchi wa kubangua korosho kwa lengo la kuharakisha uandaliwaji wake tayari kwa mauzo.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alitangaza nyongeza ya bei ya kununulia zao hilo kufikia Sh 3,300 kwa kilo huku akiliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kukusanya na kubangua korosho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye kikao kuhusiana na maonesho ya siku nne ya bidhaa za viwanda vya ndani yanayoanza leo Sabasaba wilayani Temeke, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda alibainisha kuwa uhitaji wa ubanguaji wa korosho hizo ni mkubwa.

Kakunda amesema, kwa sasa viwanda vya hapa nchini vina uwezo wa kubangua tani 40,000 kwa siku huku uhitaji ukiwa ni mkubwa zaidi hasa kwa kipindi hiki ambacho serikali inanunua zao hilo.

Alisema, kutokana na hali hiyo serikali inaendelea kuimairisha viwanda vya ndani kwa kuvijengea uwezo wa kubangua kiasi kikubwa cha korosho na wakati huo huo ikiendelea kuwasaka wazabuni hao.

Katika kuhakikisha hatua ya serikali ya kununua korosho inawanufaisha wakulima, waziri huyo alibainisha kuwa zaidi ya walanguzi 20 wa korosho za wakulima wamefikishwa mahakamani.

Alisema, wakati Serikali ikinunua korosho kwa Sh 3,300 kwa kilogramu, kuna walanguzi wamenunua korosho kwa Sh 600 na wanazipeleka kuuza kwa Serikali Sh 3,300 na vyombo vya dola vinawakamata.

Alisema:“Rais John Magufuli hakufanya kosa kununua korosho kwa shilingi 3,300 lengo lake ni mkulima anufaike, sasa hao wanaolangua kwa wakulima na kuja kuuza kwa bei ya juu lazima wakomeshwe.”

Alitoa mwito kwa walanguzi waliolangua korosho za wakulima kuwarejeshea korosho zao pamoja na fedha ili wakulima hao wakaziuze wenyewe na kunufaika na uamuzi wa Rais Magufuli wa kuuza korosho kwa bei ya Sh 3,300 kwa kilo.

Waziri Kakunda akizungumzia zaidi kuhusiana na Manesho hayo ya Biashara yanayoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (Tantrade) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) chini ya kaulimbiu ya “Tanzania sasa tunajenga viwanda”, alibainisha kuwa yatahusisha washiriki 513.

Alisema, pia kesho kutakuwa na Kongamano la kuhamasisha uwekezaji wa kuufikia uchumi wa kati kupitia ujenzi wa uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Mwakilishi wa UNIDO nchini, Stephen Kargbo amebainisha kuwa shirika hilo limedhamiria kusaidiana na serikali katika kufikia adhma ya Tanzania ya viwanda huku akisisitiza kuwa litaendelea kusaidia na wazalishaji wa viwanda wadogo na wakubwa.

ILI Tanzania ijenge Uchumi wa Viwanda, hadi kufikia mwaka 2025 ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi