loader
Picha

Mapadri, mashehe wabanwa uwasilishaji vyeti vya ndoa

WASAJILI wa ndoa, mapadri na wachungaji wa makanisa na mashehe wametakiwa kurudisha nakala za vyeti vya ndoa kwa wakati viingizwe daftari la Msajili Mkuu wa Ndoa.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudsoni kwenye taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari. Alisema viongozi wengi wa ndoa makanisani na misikitini wamekuwa wakichelewa na wengine kutopeleka kabisa nakala za marejesho ya ndoa katika Ofisi ya Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka kila mwezi kama sheria inavyosema.

“Kwa mujibu wa Sheria ya ndoa namba 29 ya mwaka 1971 kama ilivyorudiwa mwaka 2002, kifungu cha 46 kinasema kuwa kila Msajili wa Ndoa itambidi kumpecla iliyothibitishwa ni nakala ya kweli ya ndoa zote alizoziandika katika daftari la ndoa alilonalo siku 30 baada ya siku ya mwisho ya kila mwezi,” alisema akinukuu sheria hiyo.

Alisema madhara ya kutopata marejesho hayo kwa wakati ni kukosa takwimu halisi ya ndoa zote zinazofungishwa nchini, jambo ambalo ni hatari inapokuja ukusanyaji wa takwimu za matukio muhimu ya binadamu kama vile ndoa na itasaidia kuthibitisha uhalali wa vyeti hivyo. ”

Sheria ya ndoa ipo wazi kuhusiana na viongozi wa taasisi za kidini kuleta nakala za marejesho ya vyeti vya ndoa hivyo tunawakumbusha wanaofungisha ndoa katika misikiti na kanisani kutimiza wajibu wao mapema,” alisema. Aliitaja mikoa ambayo bado ipo nyuma katika kuwasilisha nakala hizo za ndoa ofisi ya Msajili Mkuu wa Ndoa Tanzania Bara kuwa ni Mtwara, Lindi, Geita, Rukwa, Katavi, Mara na Mbeya.

Hata hivyo, alisema baadhi ya mikoa kama vile, Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga na Dodoma inajitahidi kupeleka nakala za marejesho hayo. Ofisa Mwandamizi wa Ndoa na Talaka kutoka RITA Makao Makuu, Jane Barongo alisema viongozi wa dini wakitimiza wajibu wao kwa wakati itasaidia kufanya upekuzi mtu anapokuja kusajili cheti cha ndoa ofisi hizo. “Kwa mfano mtu anapokuja kusajili cheti chake cha ndoa ya mwaka fulani na tunapogundua kuwa kitabu cha mwaka huo hakijaletwa katika ofisi zetu inakuwa ngumu kufanya usajili huo,” alisema.

WABEBA nyama kwenye machinjio na mabucha watachukuliwa hatua za kisheria ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi