loader
Picha

Tano mbaroni kwa mitambo, noti bandia

JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza limekamata watu watano wanaodaiwa ni wahalifu sugu wanaohusika na utengenezaji wa noti bandia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna alisema wahalifu hao pia walikutwa na noti bandia za Sh 2,830,000. Alisema walitiwa mbaroni baada ya vikosi hivyo kuandaa operesheni maalumu Desemba 3 hadi 4, mwaka huu ambapo walikamatwa na vifaa mbalimbali vya kutengeneza noti bandia.

Kamanda Shanna alisema Polisi walifanikiwa kuwakamata wahalifu hao baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kutoka kwa raia wema kwamba katika Mtaa wa Kiloleli B Kata ya Nyasaka katika Manispaa ya Ilemela wapo wahalifu sugu wanaotengeneza noti bandia.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo, Polisi kwa kushirikiana na Polisi kutoka mikoa jirani, kwa pamoja waliitisha operesheni maalumu Desemba 3 hadi 4, mwaka huu na kuwakamata wahalifu.

Alisema wahalifu hao walikutwa na noti bandia zilizotengenezwa katika makundi manne, la kwanza lilikuwa ni noti bandia za Sh 10,000 zilizokuwa na thamani ya Sh 2,230,000, la pili ni noti bandia za Sh 5,000 zenye thamani ya Sh 470,000, la tatu ni noti bandia za Sh 2,000 za Sh 60,000 na kundi la nne ni dola bandia 100 zenye thamani ya Dola za Kimarekani 1,400.

Aliwataja wawili waliokamatiwa Mugumu wilayani Serengeti kuwa ni Swedi Amari Mrete maarufu kama Kango (40) mfanyabiashara mkazi wa Buhongwa na Cosmas Busiga Bereka (40) fundi cherehani wa Mandu, Mwanza.

Mbali ya kukamatwa na noti hizo bandia, Kamanda Shanna alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza noti bandia. Aliwataja wengine waliokamatwa Mtaa wa Kiloleli kwenye nyumba ya kutengenezea noti hizo bandia ni Baraka Dominiko maarufu kama Mwanga (26), mfanyabiashara na mwanamke, Khadija Mussa Elias (20) ambaye ni mkulima wote wakiwa ni wakazi wa Mtaa wa Kiloleli B.

Alisema Polisi ilifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa aliyetoroka, Batisti Katumbi (40) mfanyabiashara na mkazi wa Igoma Mwanza aliyekamatwa Mto Malagarasi Kasulu, Kigoma.

WABEBA nyama kwenye machinjio na mabucha watachukuliwa hatua za kisheria ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi