loader
Picha

Wafanyabiashara wataka FCC idhibiti bidhaa

WAFANYABIASHARA mkoani Dodoma wameitaka Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) idhibiti bidhaa feki zilizo chini ya kiwango ili kulinda soko la bidhaa za viwanda vya ndani.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa biashara ulioitishwa na Tume ya Ushindani (FCC) kwa Ushirikiano na Chama cha Wenye Viwanda, Biashara na Kilimo, (TCCIA), kwa nyakati tofauti walisema, kuna sababu kudhibiti bidhaa feki kutoka nje zinazoua soko la ndani.

Mkurugenzi wa Abuu Hardware, Abdulrahmani Mwayu alisema ukaguzi wa bidhaa mipakani unatakiwa kufanyika kwa makini ili kulinda soko la ndani la bidhaa ambazo haziuziki kutoka na soko kujaa bidhaa za nje zisizo na ubora na zinazouzwa bei ndogo sababu hazilipiwi kodi.

Mwayu amesema kutokana na bidhaa kutoka nje kuingia nchini kwa njia ya panya na kuuzwa kwa bei ndogo, wazalishaji wa ndani wengi wanashindwa kuzalisha na kufanya biashara, hivyo kuua mitaji yao na kuanguka biashara.

Pia alisema wananchi wengi hawana uelewa wa tofauti ya bidhaa bora na feki wanachoangalia ni udogo wa bei, hivyo kutokana na bidhaa za ndani kuwa na bei kubwa, wananunua za nje na kusababisha za ndani zikose soko japo ni bora.

Mfanyabishara mwingine, Daud Masood kutoka Mtoha Limited alisema, FCC wanatakiwa kudhibiti mipaka ili kuzipa soko bidhaa za ndani kuuzwa na kuongeza mitaji ya waendeshaji hao.

"Wanashindwa kufanya biashara na viwanda vingi vinakufa kutokana na bidhaa feki kutoka nje kuzagaa katika soko la ndani ya nchi na hivyo hakuna ushindani katika soko," amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCC, Dk John Kaduma alisema wameamua kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa jiji hilo wajue namna tume hiyo inavyofanya kazi ya kusimamia ushindani ulio sawa katika uwanja wa biashara.

Amesema lengo la tume ni wafanyabiashara kujua sheria na haki zao na namna gani wanaweza kufanikiwa katika shughuli zao kutokana na kujua haki zao katika kufanya biashara hizo.

Alisema miongoni mwa elimu wanayotoa ni ya kampuni ndogo zenye mitaji midogo chini ya Sh bilioni 3.5 kuungana kuwa na mitaji mikubwa kwa lengo la kuzifanya ziache kuwa kampuni ndogo hadi kuwa kampuni zenye mitaji ya kati.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TCCIA Dodoma, Chavuma Harun amesema wafanyabiashara wanatakiwa kuachana na mtindo wa kufanya biashara ya kawaida badala yake, walenge zaidi kuboresha biashara zao.

Wanatakiwa kutumia elimu wanayopewa na tume hiyo kuboresha biashara zao na kuzingatia ubora wa bidhaa wanazouza kutokana na ukweli ni wajibu wao kufanya biashara ya bidhaa halisi.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda ameipongeza kampuni inayojihusisha ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi