loader
Picha

Wagombea Yanga kusailiwa leo

USAILI wa wagombea wanaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa klabu ya Yanga unatarajiwa kufanyka leo na kesho.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya habari jana, usaili huo utafanyika katika ofisi za Shirikisho hilo, Karume Ilala. Taarifa hiyo ilisema, mgombea afike na vyeti vyake halisi na uthibitisho wa uanachama wake na kwamba usaili utaanza saa nne asubuhi. Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Januarimwakani na unasimamiwa na kamati ya uchaguzi ya TFF kwa kushirikiana na uongozi wa klabu hiyo.

Nafasi sita zinatarajiwa kujazwa katika uchaguzi huo mdogo ambazo ni Mwenyekiti, makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji. Wagombea 27 walipitishwa kwenye mchujo wa mwisho kuwania nafasi hizo kwa nafasi ya Wagombea Uenyekiti ni Dk.

Jonas Tiboroha, Mbaraka, Igangula, Erick Ninga huku nafasi ya makamu Mwenyekiti ikiwaniwa na Titus Osoro, Salum Chota na Yono Kevela. Wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Islam, Benjamin Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Mussa Katabaro, Shiftu Amri, Said Baraka, Pindu Luhoyo na Dominick Francis. Wengine ni Seko Jihadhari, Ally Msigwa, Arafat Hajji, Geoffrey Mwita, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Mabula, Christopher Kashiririka, Athanas Kazige na Justin Bisangwa.

YANGA imepania kushinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi