loader
Picha

Wafanyabiashara kutoa tamko ukusanyaji kodi

Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania imeahirisha kikao kati yake na wafanyabiashara kilichokuwa na lengo la kuunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kuhusu ukusanyaji kodi.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Siliver Kiondo amesema kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kuwa, kikao hicho kingekuwa cha wazi lakini kimeahirishwa kwa sababu za usalama.

"Maafisa usalama wametushauri kuahirisha kikao hiki kutokana kuwepo kwa shughuli nyingi mjini na hivyo kuwa ngumu kusimamia usalama pande zote" amesema Kiondo.

Amesema kikao hicho kitafanyika kesho na watatoa tamko la kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli sanjari na kutoa madukudku yao.

"Lengo letu sio kuleta vurugu bali kusoma tamko kwa nia njema kabisa ya kuboresha utendaji kazi wetu" amesema Kiondo mbele ya wafanyabiashara wa maeneo ya Kariakoo jijini humo.

ILI Tanzania ijenge Uchumi wa Viwanda, hadi kufikia mwaka 2025 ...

foto
Mwandishi: James Kamala

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi