loader
Picha

Tumefungwa na timu bora- Mbabane

TIMU ya Mbabane Swallows ya eSwatini imesema imefungwa na timu bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuitakia kila la Simba katika hatua inayofuata.

Mbabane juzi ilifungwa mabao 4-0 na Simba katika mecgi ya marudiano ya hatua ya awali katika michuano hiyo na kufanya kung’olewa kwenye michuano hiyo kw ajumla ya mabao 8-1 baada ya kufungwa mbao 4-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mbabane iliwamwagia sifa wapinzani wao hao na kuwatakia kila la kheri katika hatua inayofuata. “Hongera kwa Simba Sports Club kwa kuvuka katika hatua nyingine baada ya kutufunga mabao 4-0 na kuwa 8-1 katika matokeo ya jumla. Kila la heri katika safari yenu ya Caf, tumepoteza dhidi ya timu bora zaidi. Ukiwa na ndoto kubwa mtafika mbali… Tunawapenda,” ulisomeka ujumbe huo.

Aidha, klabu hiyo imewataka radhi mashabiki wake na kuwaomba kuwa na subra kwani mpira wa miguu ndivyo ulivyo. Klabu hiyo ilitaja sababu za kufanya vibaya ni baadhi ya wachezaji wake kuwa majeruhi na wengine kuhama na kuahidi kuwafurahisha mashabiki wake siku zijazo.

Chapisho hilo liliambatanishwa na baadhi ya picha za wachezaji muhimu waliowahi kuitumikia timu hiyo na kuipa matokeo mazuri kwenye michuano hiyo. Kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi aliyeihama Mbabane mwanzoni mwa msimu uliopita na kutua Yanga, nayo ilikuwepo kuashiria bado wanaikumbuka kazi yake. “Mashabiki wa Mbabane msikate tamaa, bado tunaendelea kutengeneza timu baada ya kupoteza wachezaji wetu wazuri waliotuongoza kushinda dhidi ya timu kubwa na wengine watatu kati yao wanaendelea kupona.

YANGA imepania kushinda mchezo wake dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Hans Mloli

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi