loader
Picha

Tanesco wahamia rasmi Dodoma

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Tito Mwinuka amezindua rasmi ofi si mpya ya Dodoma na kubainisha kuwa makao makuu ya shirika hilo sasa yamehamia rasmi Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokewa katika ofisi za Tanesco, Dk Mwinuka alisema kuanzia sasa shughuli zote zitafanyika kuanzia Dodoma na huduma zote za kiofisi zitaendelea kama kawaida katika kanda saba, mikoa 29 ya Kitanesco na Wilayani.

Alisema uwepo wa serikali Dodoma huku makao makuu ya Shirika hilo yakiwa Jijini Dar es Salaam ufanisi wa kazi unaweza kuwa si mzuri. “Tukiwa Dodoma ufanisi wetu utakuwa ni mzuri, natumaini tutatoa huduma bora zaidi kwa wananchi,” alisema.

Alisema ujio wa serikali Dodoma utasababisha ujenzi wa majengo mengi yakiwemo ya serikali na huduma ya umeme itahitajika sana. Dk Mwinuka alisema katika awamu ya kwanza, watumishi 30 wameshafika Dodoma kutoka makao makuu Dar es Salaam. “Tutajenga jengo jipya hapa Dodoma ambalo litawapokea watu wote watahaohamia Dodoma,” alisema.

Alisema jengo hilo jipya litajengwa na bajeti yake itatengwa mwaka ujao wa fedha na sasa kinachofanyika ni matayarisho ya mwanzo fedha zitakapokuja. Wakati huo huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, January Makamba jana alikagua eneo litakapojengwa ofisi za wizara hizo huku akibainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itakuwa na ofisi zake kwenye makao makuu ya serikali. Akizungumza katika mji wa serikali eneo la Mtumba alisema ofisi yake ina ekari nane kwa ajili ya ujenzi wa ofisi.

Alisema wataanza na ujenzi wa jengo dogo la muda ili likikamilika watumishi wahamie. “Rais ametoa fedha kwa kila Wizara, tuko kwenye mchakato kwa kumpata mjenzi, ikiwemo wakala wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Suma JKT,” alisema.

Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais ni ofisi ya pili kubwa kiserikali lazima waoneshe dhamira ya kuhamia haraka Dodoma na kutakuwa na mpango wa kupendezesha mazingira katika mji wa serikali.

“Sisi tunasimamia Muungano ushiriki wa Zanzibar utakuwepo na kutokana na hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepata ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zake. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joseph Malongo alisema michoro ya jengo hilo imetayarishwa na Wakala wa Majengo (TBA) na jengo la chini litakuwa na mita za mraba 1,050.

SERIKALI mkoani Songwe imewataka wakulima wa zao la alizeti kubadilika ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi