loader
Picha

Staa Yanga awapinga wanaomponda Kindoki

Kiungo wa zamani wa Yanga Salvatory Edward ameingilia kati suala la kipa timu yake hiyo ya zamani Claus Kindoki.

Kindoki aliyeletwa Yanga na kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango kibovu anachoonyesha tangu alipojiunga na timu hiyo akitoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Kipa huyo alisajiliwa kama chaguo la kwanza baada ya klabu hiyo kuachana na Youthe Rostand ambae aliachwa kwa kwa kuwa aliruhusu mabao mengi ya kizembe.

Kindoki amejikuta akifungwa mabao rahisi kwenye ligi na mechi za kirafiki na hadi sasa ameruhusu mabao 10.

Hata hivyo Salvatory Edward aliyewahi kutamba na Yanga na Taifa Stars katikati ya miaka ya 1990 mpaka katikati ya miaka ya 2000, ameibuka na kuisihi klabu yake hiyo kuwa nyuma ya kipa huyo kwani tayari wameshamsajili.

“Kindoki sio kipa mbaya ingawa sio wa kiwango cha kuitwa wa kulipwa; lakini tayari Yanga imeshamsajili , hivyo wanachotakiwa ni kumuunga mkono tu kwa sasa, kumlaumu watamuondolea kabisa hali ya kujiamini na wao sasa hivi wamebakiwa na makipa wawili tu, kwani Beno Kokalonya wanasema amegoma.

“Binafsi sipendi na lawama wanazompa hata kama ni kipa wa kawaida lakini ndio tayari wako nae, wanapaswa kumuunga mkono tu na sio vinginevyo,”alisema Edward aliyetamba kwa jina la Dokta wakati akimudu vyema nafasi ya kiungo.

Tuzo Mapunda SIMBA imeanza vyema msimu huu baada ya kuifunga ...

foto
Mwandishi: Clecence Kunambi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi