loader
Picha

Matola- Yanga harakisheni

YANGA wanamtaka Ally Mtoni ’Sonso’ lakini kocha wa timu hiyo Selemani Matola amewaambia hawana budi kuharakisha kama kweli wanahitaji huduma ya beki huyo kinyume chake hawatakuwa tayari kumuachia.

Matola kiungo wa zamani wa Simba na Taifa Stars amesema Yanga wakienda siku moja kabla ya usajili kufungwa haitakuwa rahisi kumuachia kwa sababu hawatakuwa na nafasi ya kupata mbadala wa beki huyo.

“Soka ni maisha yake kama wanamuhitaji waje haraka sisi hatuwezi kumzuia, lakini wakichelewa hatutamuachia kwani muda wa usajili utakuwa umepita na sisi tutakosa mbadala wake,”amesema Matola.

Matola alimwagia sifa beki huyo wa kati kwa kusema ni mtu asiye kuwa na mambo mengi lakini anayetekeleza vyema majukumu yake ya ukabaji kama beki.

“Sonso ni kama alivyokuwa Amri Said’Stam’, hana mambo mengi uwanjani lakini anayetimiza wajibu wake vizuri katika kuzuia, akisema hauendi jua hauendi kweli,”amesema Matola.

Amesema kama Yanga watafanikiwa kumsajili beki huyo ataweza kushirikiana vizuri na mabeki wengine wa timu hiyo Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu’Ninja’ na Andrew Vicent’Dante’.

KABLA ya Yanga kukutana na As Vita ya DR. Congo ...

foto
Mwandishi: Clecence Kunambi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi