loader
Picha

'Wateja FBME muwe na subira'

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewataka wateja waliokuwa na amana zao katika benki iliyositisha huduma zake ya FBME kuwa na subira, huku taratibu za kulipwa fedha zao zikiendelea.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua lini wananchi wenye fedha zao katika benki ya FBME watalipwa fedha zao.

Akifafanua zaidi amesema suala la kulipa amana za wananchi mara baada ya benki hiyo kusitisha shughuli zake lipo chini ya Bodi ya Bima ya Amana.

Alisema taasisi hiyo imepewa jukumu hilo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye ndiye msimamizi wa taasisi zote za fedha ikiwemo benki.

Alisema utaratibu wa kuwalipa amana za wateja unaendelea awamu kwa awamu kulingana na viwango vya fedha za mteja.

Alisema wapo wateja wenye akaunti kuanzia Sh milioni 1.5 wamekuwa wakilipwa fedha zao kwa nyakati tofauti na wale wenye kiwango kikubwa zaidi watalipwa fedha hizo baada ya kukamilika kwa mchakato wa ufilisi.

''Benki ya FBME imesitisha shughuli zake na sasa ipo katika mchakato wa kulipa madeni ya wateja wake kwa hivyo wananchi ikiwemo walioguswa na kadhia hiyo kuwa na subra,'' amesema.

Dk Mohamed alisema serikali inafuatilia suala hilo na kujua hatma yake kwa sababu watu walioathirika wanatoka Zanzibar katika moja ya tawi la benki hiyo.

Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, masuala yote ya fedha na sarafu na benki yanasimamiwa na BoT.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi