loader
Picha

Wagonjwa saratani Ocean Road kutibiwa moyo

TAASISI ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam imeanzisha huduma mpya nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki ya kutoa matibabu ya moyo kwa wagonjwa wenye saratani.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Julius Mwaisalage alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma hiyo. Alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka Shirika la Nyuklia duniani watatoa huduma hiyo kwa wagonjwa husika. “Tutapima moyo unavyofanya kazi, tutaangalia kama umeathirika kwa tiba iliyopo ya saratani.

Mara nyingi wagonjwa wa saratani wanaopata tibakemia wanadaiwa kuathiriwa moyo,” alisema. Alisema kupitia utaalamu huo mpya na vifaa walivyo navyo, watapunguza athari za wagonjwa wanaotibiwa na tibakemia pamoja na rufaa za kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Alisema miaka mitatu iliyopita wamepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwani mwaka 2015 walipeleka wagonjwa kati ya 150 na 200, kipindi hicho pia upatikanaji wa dawa za saratani ulikuwa ni asilimia nne na sasa ni 95.

Alisema taasisi hiyo ina vifaa vingi vya kisasa vinavyorahisisha kutoa huduma kwa wagonjwa. Daktari Bingwa wa Mionzi ya Nyuklia ambaye ni Meneja wa Kitengo cha Nyuklia, Tausi Maftah alisema dawa wanazopewa wagonjwa wa saratani zinaweza kuwapa wagonjwa athari. “Sasa hivi tutaweza kugundua haraka kama kuna tatizo lolote ili mgonjwa abadilishiwe dawa au apumzishwe kidogo,” alisema.

Alisema hata kwa wagonjwa wengine wenye matatizo ya moyo, huduma hiyo mpya itasaidia kugundua tatizo la mishipa ya moyo kuziba. “Kipimo hiki kitasaidia kugundua wanaopaswa kwenda upasuaji au kupata dawa tu,” alisema.

SERIKALI mkoani Songwe imewataka wakulima wa zao la alizeti kubadilika ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi