loader
Picha

Maofisa Katiba na Sheria wapitia utekelezaji haki za walemavu

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju (pichani) amesema serikali imeridhia mkataba wa kimataifa wa kutetea haki za watu wenye ulemavu wenye lengo la kuwalinda watu wa kundi hilo.

Aidha, amewaagiza wataalamu katika ofisi yake kuhakikisha wanakuwa na mfumo mzuri wa kupokea taarifa za utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa ili kurahisisha uandikaji wa taarifa.

Mpanju aliyasema hayo wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili cha kupitia rasimu ya taarifa ya nchi juu ya utekelezaji wa haki za watu wenye ulemavu. Alisema serikali iliridhia mkataba huo wa umoja wa mataifa kwa lengo la kulinda na kuteteka kundi la watu wenye ulamavu ambalo lilikuwa limesahaulika kwa miaka mingi.

“Mwaka 2009, serikali iliridhia mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu, haikuridhia kama mapambo bali ni katika kuchukua hatua za kulinda watu wenye ulemavu,” alisema.

Alisema katika kutekeleza hilo, serikali imeweka mifumo ya sheria na utendaji ambayo inalinda haki za watu wenye ulemavu. “Kuna sheria nyingi ambazo zinatetea haki za watu wenye ulemavu, mfano hivi karibuni tutatoa mkakati wa ujenzi ambao utalazimisha majengo ya umma yanazingatia mahitaji ya ufikikaji,” alisema.

Aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanapitisha taarifa yenye uhalisisa yenye ushahidi halisi na kusisitiza kuwa serikali imefanya mambo makubwa katika kutekea na kulinda haki za watu wenye ulemavu.

Aidha, Mpanju alimuagiza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Haki za Binadamu, Mkasori Sarakikya kuhakikisha wanakuja na mfumo ambao utakuwa ukipokea taarifa ya kile kilichofanyika kwenye mikataba yote ambayo serikali inawajibika kutoa taarifa. Naye, wakili Gidion Mkendesi aliipongeza serikali kwa kupiga hatua kubwa katika kutetea na kulinda haki za watu wenye ulemavu.

WABEBA nyama kwenye machinjio na mabucha watachukuliwa hatua za kisheria ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi