loader
Picha

Mbarawa ataka wanaohujumu maji wasakwe

WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amevitaka vyombo vya dola kushirikiana na maofi sa wa Shirika la Maji Dar es Salaam (DAWASA) na watendaji wa serikali za mitaa, kuwasaka wanaohujumu mradi wa maji Kata ya Kiwalani, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.

Katika mradi huo wenye miezi michache tangu uzinduliwe, watu wasiojulikana wamedaiwa kuingiza maji machafu katika mabomba ya Dawasa wananchi wakatae kutumia maji hayo.

Akizungumza jana katika mkutano na wananchi wa Kata ya Kiwalani uliofanyika katika viwanja vya soko la Bombom kwa lengo la kujua kero katika mradi huo, Mbarawa alisema mradi huo umetumia fedha nyingi ambazo ni kodi za wananchi hivyo hawataweza kumvumilia wala kumbembeleza mtu yeyote anayeuhujumu. “Naagiza vyombo vya usalama, Polisi mpo hapa naomba mshirikiane na Dawasa na viongozi wa serikali za mtaa kuwasaka.

Tutawakamata kwa sababu vyombo vyetu vya dola viko vizuri na tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria wachukuliwe hatua,” alisema Profesa Mbarawa. Wakitoa kero zao mbele ya Waziri Mbarawa, wananchi wa Kata hiyo walilalamikia maji kutoka machafu, yenye harufu kali na kuleta adha kubwa ya upatikanaji wa maji safi.

Akizungumzia kero hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja alisema baada ya kupata taarifa za kuchafuliwa maji walifanya uchunguzi wa bomba lao na kubaini hakuna sehemu linakovuja hivyo kuleta hisia kuwa ni hujuma zinazofanywa na watu waliokuwa wanapinga mradi huo kwa maslahi yao binafsi. “Wakati tunaleta mradi huu tulikumbana na mapingamizi ya watu wakidai hawana shida ya maji lakini tuliwaeleza suala la kuleta maji safi na salama ya gharama nafuu ni jukumu la serikali na tukaleta mradi sasa wanauhujumu ili wananchi waukatae,” alisema Luhemeja.

“Tumeanza uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili kuwabaini wanaofanya mchezo mchafu kuhujumu mradi huo,” alisema. Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji wa Dawasa, Aron Joseph alisema kuna hisia wanaochafua maji hayo ni watu waliokuwa na miradi ya kuuza maji katika kata hiyo kabla Dawasa haijapeleka mradi huo wa maji safi. Alisema hisia hizo zimekuja baada ya timu ya Dawasa kuchukua sampuli ya maji katika mabomba ya kata hiyo na kuthibitisha kuwa yamechafuliwa lakini walipofuatilia bomba lao hapakuwepo na sehemu yoyote inayovuja maji.

ZIKIWA zimesalia siku chache kwa Wizara ya Nishati kuwasilisha bungeni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi