loader
Picha

MOI waokoa maisha ya aliyechomwa kisu

MADAKTARI bingwa wa Taasisi ya Mifupa (MOI) wameokoa maisha ya Mwalami Saidi (26), kijana mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam ambaye alijeruhiwa kwa kuchomwa kisu mgongoni na watu wanaosadikika kuwa ni wezi.

Mwalami alichomwa kisu Desemba 3, mwaka huu, saa 4 usiku akitoka kazini na alisaidiwa na msamaria mwema, dereva wa pikipiki (bodaboda). Dereva huyo alimpeleka Hospitali ya Rufaa ya mkoa Amana ambako alipewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kisha kuhamishiwa MOI alikopasuliwa kuondoa kisu.

Baada ya kuokolewa, Mwalami aliwashukuru madaktari wa MOI kwa kufanikisha upasuaji huo kwani alikua anapata maumivu makali. Upasuaji wa kutoa kisu kwenye mgongo wa Mwalami umefanywa na jopo la madaktari bingwa wanne kwa muda wa saa mbili.

Madaktari bingwa waliofanya upasuaji huo walisema kisu hicho kilikuwa kinahatarisha maisha yake hivyo alihitaji upasuaji wa dharura kwani kilikuwa kinaathiri mgongo na viungo vingine kama mapafu na angeweza kufariki.

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga ameonesha kukerwa na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi