loader
Picha

Tanzania yapata madaktari bingwa 2 upasuaji wa ubongo

KWA mara ya kwanza Tanzania imepata madaktari bingwa wanawake wa upasuaji ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Madaktari hao ni Aingaya Kaale na Happiness Rabiel ambao wamesoma katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), na kufanya mafunzo kwa vitendo katika taasisi ya MOI.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi, madaktari hao bingwa wamehitimu na kuthibitishwa katika mahafali yaliyofanyika juzi katika Jiji la Kigali, Rwanda. “Mahafali hayo yalisimamiwa na Chuo cha Madaktari Bingwa wa Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini (COSECSA).

“COSECSA hawana chuo maalumu nchini ila wana vituo vya kufundishia, na MOI ni kimojawapo, hivyo walikuwa chini ya MUHAS, MOI na COSECSA,” alisema. Mvungi alisema baada ya kuhitibu sasa taasisi hiyo imekuwa na jumla ya madaktari 10 wa matatizo hayo. Alisema madaktari hao wamesoma miaka sita, miaka mitatu ikiwa ya Shahada ya Uzamili ya Upasuaji (General Surgery) na miaka mitatu mingine ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (Msc Neurosurgery).

Alisema pamoja na madaktari hao wanawake, daktari bingwa mwingine mwanamume wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu Raymond Makundi pia amehitimu masomo yake. Alisema madaktari bingwa wengine wa mifupa walikuwa wanafanya mafunzo ya ubobezi wa juu wa upasuaji wa mifupa ya satori ambao ni Dk Bryson Mcharo na Dk Msami Ngowi.

SERIKALI mkoani Songwe imewataka wakulima wa zao la alizeti kubadilika ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi