loader
Dstv Habarileo  Mobile
Schalke 04 kuwakabili vinara Borussia Dortmund Jumamosi

Schalke 04 kuwakabili vinara Borussia Dortmund Jumamosi

Kila inapofika wikendi basi wapenzi wa Soka wanajua tayari ni muda mwingine wa burudani yao wanayoipenda zaidi.

Shauku ya kuwaona wachezaji wanaowapenda na kandanda la kuvutia, mahali sahihi ni ST World Football ambao watakuonyesha kandanda muda wote.

Ligi mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Bundesliga zinaendelea tena wikiendi hii ambapo Schalke 04 watakuwa nyumbani kuikabili Borrusia Dortmund ambao ni vinara wa ligi hiyo ua Ujerumani.

Timu hizo zinakutana kesho Jumamosi huku rekodi zikionesha kuwa, Borussia Dortmund wamefunga jumla ya mabao 37 huku Schalke wakiwa wamefunga magoli 14 tu katika michezo 13 ya ligi na wanashikilia nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ambayo Dortmund ndio kinara.

Katika mchezo huo ambao utarushwa utarushwa mubashara kupitia ST World Football HD saa 11:30 jioni kesho, Dortmund wanaonekana kukamilika katika safu ya kiungo na ushambuliaji ambayo inaongozwa na Marco Reus.

Reus amefunga magoli tisa na kusaidia mengine matano huku kinara wa magoli Paco Alcacer akiwa na magoli 10 ambapo saba ameyafunga akitokea benchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/32ec3bf2db22895895d77d025d2accc0.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi