loader
Taji la Miss World laenda Mexico

Taji la Miss World laenda Mexico

MISS Mexico, Vanessa Ponce de Leon ndiye aliyetwaa taji la mrembo wa dunia, Miss World 2018, katika fainali za shindano hilo zilizofanyika Sanya, China.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo kutoka Thailand, Nicolene Pichapa na mrembo wa Tanzania, Queen Elizabeth Makune aliyepewa nafasi ya kung’ara akiachwa mbali.

Katika shindano hilo, mrembo huyo kutoka Mexico pia aliibuka Miss World kutoka bara la Amerika na mrembo wa taji mwenye malengo.

Mrembo kutoka Uganda, Quiin Abenakyo alitwaa taji la Miss World Afrika.

Warembo wengine walioshinda Miss World katika mabara yao ni Miss World Ulaya kutoka Belarus, Maria Vasilevich, Miss World Caribbean kutoka Jamaica, Kadijah Robinson, Miss World Amerika kutoka Mexico, Vanessa Ponce de Leon, na Miss World Asia and Oceania kutoka Thailand, Nicolene Pichapa Limsnukan Miss Nepal Shrinkhala Khatiwada alitwaa taji la Multimedia & Beauty with a Purpose.

Miss Ufaransa Maëva Coucke alitwaa taji la Top Model Winner, Miss Japan Kanato Date alitwaa taji la mrembo mwenye kipaji na Miss Marekani Marisa Butler alitwaa taji la mwanamichezo.

Taji la Miss World 2017 lilikuwa linashikiliwa na Miss China Manushi Chhillar ambaye hata hivyo nchi yake iliishia katika 30 bora.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5c37bf531512b83cda0b2ecd342dff23.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi