loader
Picha

Wanafunzi 500,000 wachaguliwa kidato 1

JUMLA ya wanafunzi 599,356 kati ya wanafunzi 733,103 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari katika shule mbalimbali.

Aidha wanafunzi 133,747 waliofaulu wanakosa nafasi hiyo kutokana na uhaba wa madarasa. Kwa takwimu hizo, uchaguzi wa wanafunzi mwaka 2019 umeshuka tofauti na mwaka huu wa 2018 ambapo walichaguliwa wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31 kujiunga na kidato cha kwanza.

Akitangaza matokeo hayo Dar es Salaam jana ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ambao ni 599,356 ni sawa na asilimia 81.76 ya waliofaulu huku wale waliokosa ni asilimia 18.24.

Jafo alisema jumla ya mikoa tisa pekee kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara ndio iliyochukua wanafunzi hao 599,356 kwa asilimia 100. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Geita, Kilimanjaro, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Singida na Songwe.

Alitaja mikoa yenye uhaba wa vyumba vya madarasa na idadi ya wanafunzi waliofaulu ni pamoja na Arusha ambayo walifaulu wanafunzi 33,055 waliochaguliwa ni 14,316, waliokosa 18,719. Dodoma waliofaulu 31,103 waliochaguliwa ni 25,057 waliokosa 6,046, Iringa waliofaulu 21,314 waliochaguliwa ni 18,540 waliokosa ni 2,774, Kagera jumla waliofaulu wanafunzi 39,545, waliochaguliwa ni 25,498 waliokosa ni 14,047.

Kigoma waliofaulu ni 25,704, waliochaguliwa 13,526 waliokosa 12,178, Lindi waliofaulu 13,074, waliochaguliwa ni 12,137 waliobaki ni 937, Mara waliofaulu ni 35,804 waliochaguliwa ni 19,439 waliobaki ni 16,363. Mbeya waliofaulu ni 34,403 waliochaguliwa ni 288,008 waliokosa ni 6,395, Pwani waliofaulu ni 23,170 waliochaguliwa ni 18,439 waliokosa ni 4,731, Rukwa waliofaulu ni 15,193 waliochaguliwa 9,015 waliokosa ni 6,178 .

Tabora jumla waliofaulu ni 29,077 waliochaguliwa ni 17,868 waliobaki 11,209 Tanga jumla waliofaulu ni 35,728 waliochaguliwa 30,328 waliobaki ni 5,400, Manyara jumla waliofaulu ni 21,453 waliochaguliwa 16,061 waliobaki 5,392. Shinyanga jumla waliofaulu ni 23,391 waliochaguliwa 17,120 waliobaki 6,271, Katavi jumla waliofaulu ni 7,967 waliochaguliwa 6,718 waliobaki 1,249, Njombe waliofaulu ni 15,507, waliochaguliwa ni 12,335 waliobaki 3,172,Simiyu waliofaulu ni 24,983 waliochaguliwa 12,299 waliobaki ni 12,684.

Jafo amewaagiza wakuu wa mikoa ambayo haijakamilisha ujenzi wa miundombinu hasa ya vyumba vya madarasa kuhakikisha wanakamilisha hadi kufikia mwezi Februari, 2019 ili wanafunzi waliokosa wapate nafasi katika awamu ya pili ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2019.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba wanapata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, nimeshatoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019,” alisema Jafo.

Jafo amesisitiza kuwa walezi na wanafunzi ambao watakosa nafasi katika awamu ya kwanza ya uchaguzi kuwa wavumilivu wakati mikoa inajiandaa kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wote kuanza masomo ya kidato cha kwanza. Aidha amewaomba wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kushirikiana na Wilaya, Halmashauri na shule, kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa, wanahudhuria na kubaki shuleni hadi watakapohitimu elimu ya sekondari.

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi