loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jaji Mkuu wa Kenya, mkewe wapata ajali

J AJI Mkuu wa Kenya, David Maraga na mkewe Yucabeth Nyaboke, wamenusurika kifo baada ya gari lao kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Toyota Saloon.

Ajali hiyo iliyotokea jana asubuhi mjini Nakuru, ilisababisha wanandoa hao kupata majeraha na kuwahishwa katika Hospitali ya War Memorial mjini humo kwa matibabu ya awali kabla ya kuhamishiwa Nairobi kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa Polisi, Jaji Maraga na mkewe walikuwa wakienda kanisani na ndipo gari hilo lilipoingia barabra kuu kutokea pembeni bila kuchukua tahadhari na hivyo kusababisha ajali. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Nakuru, Ziro Arome alisema hali za majeruhi zimeendelea kuimarika.

Akiwa katika hospitalini Nakuru, Jaji Mkuu Maraga alivieleza vyombo vya habari kuwa yeye na mkewe hali zao zinaendelea vizuri na wangesafirishwa kwenye Hospitali ya Nairobi kwa uchunguzi zaidi wa afya zao. Polisi walisema Jaji Mkuu Maraga alipata majeraha kwenye paji la uso wakati mkewe alikuwa ameumia shingo, huku dereva wao, Jonathan Kigen akipata majeraha kichwani na alipatiwa matibabu Nakuru na kisha kuruhusiwa.

BARAZA jipya la mawaziri nchini Burundi, lililoteuliwa na Rais mpya, ...

foto
Mwandishi: Nairobi, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi