loader
Picha

Kumiliki gari si kigezo cha kuwa dereva

MSIMU wa sikukuu za mwisho wa mwaka umewadia. Siku mbili zijazo duniani kote kwa Wakristo watakuwa wanasherehekea Sikukuu ya Kuzaliwa Mwokozi Yesu Kristo, ambayo huitwa Sikukuu ya Kristimasi au Noeli.

Sambamba na sikukuu hiyo ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Kristo yapata miaka 2,000 iliyopita, pia ni majira ya mwisho wa mwaka ambapo wananchi duniani kote husherekea kumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya.

Sikukuu hizo huwa kwa kawaida zinaambatana na tamaduni mbalimbali za watu kulingana na maeneo yao. Wengi husafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya kuungana na ndugu zao na kusherekea kwa pamoja matukio hayo muhimu ya kujamii na kiimani pia. Sasa basi kwa wale wanaosafiri na familia kwenye magari binafsi, wakati huu wa sikukuu, hamna budi kuwa makini.

Kumbukeni kwamba kumiliki magari au gari hakukufanyi kuwa dereva wa masafa marefu au mafupi, ni lazima vigezo na masharti ya udereva yakazingatiwa na sio kila mtu ni dereva ilimradi tu alijifunza kuendesha gari vichochoroni na kupata leseni kwa njia za panya akawa dereva wa familia. Kufanya hivyo ni kuweka rehani roho za familia husika, kwani udereva ni lazima uwe na vigezo na pia huweze kutambua kuwa na stamina na kuifahamu barabara na alama zake ipasavyo ili uweze kuendesha kwa tahadhari na kujali watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Lakini kama wewe ni dereva ila huna uzoefu wa kuendesha nyakati za usiku ni vyema ukaendesha mchana wakati kuna mwanga wa kutosha pia pata muda wa kutosha kupumzika. Cha kuzingatia ni kwamba tambua kuwa gari unalotumia lina idadi ya watu inayopaswa kupakiwa na sio kubeba abiria kwa maana ya wanafamilia wengi kupita uwezo wa gari, kwani ni lazima wote wanaopanda wafunge mkanda wakati wote wa safari.

Nasema hayo kwa sababu zipo baadhi ya familia wanadhani kuwa na gari basi ni kupakia familia yote hata kama uwezo wa gari ni mdogo na wengine wanadhani kuwa watoto wanaweza kupakatwa tu au wakaachwa wanachezacheza na wakati mwingine wanarukaruka ndani ya gari.

Jambo hilo sio sahihi hata kidogo! Ni hatari ni lazima kila abiria akafunga mkanda na tutambue kuwa hata watoto wanapaswa kufungwa mkanda na kwa wale watoto wadogo chini ya miaka miwili kuna viti vyao maalum vinavyowekwa ndani ya gari kwenye siti za nyuma na kisha unawafunga mikanda. Tuache tabia ya kubeba watoto wakubwa au wadogo ndani ya magari na kutowafunga mikanda wakati wa safari ndefu au fupi kwani ni hatari.

Lakini pia kama familia ina magari lakini haina madereva wazoefu ni vyema kukodi dereva unayemuamini ili afanye safari yenu iwe salama kwani kuendesha gari kama sio dereva unaweza kuhatarisha maisha kwani wakati mwingine vyombo hivyo vya moto huwa vinakuonesha tatizo la gari linapotokea.

 

Siku mbili zilizopita nilishuhudua ajali baina ya pikipiki na daladala ...

foto
Mwandishi: Ikunda Eric

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi