loader
Picha

Irene Mbowe: Kungwi wa kisasa aliyeponya ndoa nyingi

IRENE Mbowe (42), ni mwanamama wa kitanzania anayevuma zaidi kwenye mitandao ya kijamii na kwenye majukwaa mbalimbali kutokana na mijadala anayoongoza au kushiriki yenye mafundisho ya mauhusiano yaliyosaidia kubadilisha mitazamo na mingine imenusuru ndoa zilizokuwa hatarini kuvunjika. Huyu kweli ni mwanamke wa shoka, na nina amini kila mwanamke anaweza kuwa mwanamke wa shoka, pale atakapoamua kufanya jambo kwa moyo na kuondoa uoga. Hapa duniani kila jambo linawezekana, tatizo liko kwetu sisi wenyewe kutanguliza fikira za kushindwa au kusita kufanya jambo kwa kuogopa litapokelewaje au utaonekanaje iwapo unachokusudia kukifanya kitashindikana.

Baadhi ya mambo yaliyomfanya Irene au kwa jina maarufu, ‘Mama Neema’ au Kungwi Lao’, kujulikana ni uwezo wake wa kutawala jukwaani kwenye mitandao ya kijamii anapoweka picha za video au sauti za maneno fupi fupi au ndefu zinazoigiza matendo mbalimbali yanayofanywa na jamii ikiwemo mawasiliano baina ya wanadoa. Uwezo wake mkubwa ndio uliomfanya ajulikane na kuwa mfano na mtu maarufu anayependwa zaidi hivi sasa kusikilizwa, au kutazamwa na wasomi, wenye pesa na hata wasio na pesa , na kwa ujumla makundi yote ya watu yanamwangalia kungwi huyu kama kioo katika jamii ya sasa.

Baadhi ya video fupi fupi zenye ujumbe kwa wanadoa zilizompatia umaarufu mkubwa Irene ni ‘Mama Neema’ ambayo inaonesha jinsi mwanamke alivyo na upendo wa mumewe na video hii imependwa na kuongeza mashabiki wake hasa wanaume.

HabariLeo lilimtafuta Irene na kufanya nae mahojiano kuhusu maisha na kazi yake ambaye alisema amefanya kazi yake ya ukungwi kwa miaka 10 sasa akiwa ameokoa zaidi ya ndoa 14 zilizokufa huku akiokoa nyingine 161 zilizokuwa kwenye hali ya kufa na nyingine 16 alizishauri zikatafuta muafaka makahamani. Irene alianza kwa kusema “Unajua niliolewa mdogo sana nilikuwa na miaka 20 tu wakati ule mume wangu alikuwa na miaka 26 ndio kwanza nilikuwa nimemaliza kidato cha nne.

“Sikuwa na kazi ya maana bali nilijishughulisha na biashara ndogo ya kuuza sambusa, niliifanya kazi ile kwa uwaminifu mkubwa, mume wangu akaona kumbe nina akili akanifungulia genge, nikawa nauza nyanya, nazi, vitunguu, mboga mboga maisha yakaendelea,’’. Anasema wakati akiuza genge aliweza kupata faida ya Sh 45,000 wakati huo wasichana wasomi ambao walikuwa wakifanya kazi ya Ukatibu Muktasi walikuwa wanalipwa shilingi 80,000 akaona kumbe anaweza kupata nusu ya mshahara wao, basi akaendelea kufanya biashara hiyo kwa uaminifu. “Nikawa na genge na sambusa sikuacha kuuza, napika sambusa nauza zinaisha alafu ninaendelea na shughuli nyingine za kuhudumia familia na pia nikatenga muda wa kutumika kanisani na muda wa kumhudumia,” anasema Irene.

Ukungwi ulijifunzia wapi?

Nilipomuuliza alijifunzia wapi Ukingwi, Irene aliangua kicheko, “ haaaaa!kumtegemea Mungu kuna faida, natumia muda mwingi kusoma Biblia na kutafakari Neno la Mungu, ukisoma Biblia utapata maarifa na utajua vitu vingi hata kukabiliana na changamoto, kwenye kitchen party nyingi zinafundisha jinsi ya kukatika, jinsi ya kumuandaa mwanaume na mambo mengine kama hayo, lakini hawamfundishi bibi harusi kukabiliana na changamoto za ndoa.

“Ndio maana ndoa nyingi zinavunjika, nilitafakari hilo nikaona kuna jambo la kufanya kiimani kwa hao mabibi harusi wapya kabla hawajaingia kwenye ndoa, mwaka 2010 nikaanza rasmi kuwafunda watu kiimani kwa kutumia mistari ya Biblia, nazunguza nao unakuta mtu amekata tamaa lakini unazungumza nae, unamfariji mpaka unamrudishia tabasamu lake hata kama analia.’’

Irene anaendelea kusimulia kuwa alifanya hayo kwa uaminifu mkubwa, akaanza kujulikana zaidi na watu wakamwamini kisha akaendelea kutoa ushauri na kadri muda ilivyosonga akagundua kuna haja ya kuandaa siku ya kutoa mafunzo kwa mabibi harusi watarajiwa hivyo akaandaa kitchen gala ambayo anasema ilimkutanisha na watu wengi.

“Tuliandaa kitchen part mbali mbali nikawa napewa muda naongea basi watu wengi wakavituiwa na mimi , ingawa wapi pia walionidharau na kuniona Malaya lakini sikukata tamaa, kupitia mafundisho yangu hadi watumishi wa Mungu wakaanzakunialika kwenye makongamano kutoa ushauri na mafundisho.” Mumeo anasapoti kazi yako? Irene anasema mwanzoni nilipata tabu, alikuwa hapendi, anakasirika, alikuwa anamuona kama kahaba na kwa nini ajitangaze kungwi ili hali yeye ni mke wa mtu.

“Lakini siku zote mimi nina utaratibu wangu wa maisha na ninasimamia kanuni yangu inaitwa N-4 ikiwa na maana, najipenda, najiheshimu, najithamini na ninajituma, sikuacha kufanya wajibu wake kwangu kama mke, sikuacha kujiheshimu, kujipenda na kujithamini mwisho wa siku matunda ya kazi yangu aliyaona.”

Anasema kupitia kazi yake hiyo ameweza hata kumsaidia majukumu mengine nyumbani na sasa anapata msaada na ushauri wa mumewe kwa asilimia 100. “Siku za nyuma alikuwa akisikia neno kungwi anakasirika kabisa, lakini sasa hivi nikiongozana nae anaweza kumuita mtu na kumwambia unamuona kungwi, wakati siku za nyuma kuniita kungwi ilikuwa shida.” “Ila bado kuna kitu kimoja ambacho bado kinamkera hajakikubali mtu amuite baba Kungwi, haaaaa yewomiii, hapendi chaa anakasirika kabisa, hataki kuitwa baba Kungwi, haaaaa,” anasema Irene.

Vipi kuhusu Mama Neema ‘Kipereto, Mang’aa’? Akizungumzia video zake za mafunzo maarufu kama mama Neema, Irene anasema imempatia umaarufu mkubwa na mashabiki wengi na kikubwa ni ndoa nyingi zimepona.

“Kupitia Mama Neema ndoa nyingi zimepona, kikubwa wanandoa wengi wamejifunza jinsi ya kuzungumza na wenzi wao, sio mke unaongea kama unaongea na nani sijui lazima uwe na adabu acha kuongea kama Mama Neema ,Mang’aa,”anabainisha Irene. Anasema wazo la kutengeneza ujembe huo aliangalia maisha ya ndoa nyingi na kugundua kuwa zipo zilizovunjika na baadhi yao makosa ni ya wanawake hawajui kubembeleza au kumhudumia mume bali hufanya mashindano na mwisho wake ni kuvunjika.

“Nilijaribu kuangalia ndoa nyingi zinavunjika kwa vile wanawake wa siku hizi hawajui kubembeleza, wanaume wengi wakiafrika hususani watanzania wanapenda kubembelezwa, kujaliwa, kudekezwa bahati mbaya wanawake wa siku hizi kubembeleza hawajui, hawajui waongee vipi na mume au mpenzi wake, kuna lugha laini ambayo unaweza kutumia kwa mume au mpenzi wako akakusikiliza.

“Ukiangalia kuna Mama Neema Kipereto na Mama Neema mke mwema, mke mwema ataongea kwa upendo, atamuombea mume/mpenzi wake, tofuati na mama Neema Kipereto yeye kazi ni kuamkasirisha na kuongea kwa ukali, wanawake wengi wababe siku hizi, hivyo natumia sanaa hiyo kuwakumbusha wanawake wajibu wao, pamoja na utandawazi asili yetu itabaki kuwa asili yetu, utandawazi usitupoteze, mwanamke ni lazima unyenyekee.

Changamoto zipi unakumbana nazo? Changamoto ninayokumbana nayo ni kushindwa kujigawa hasa misimu ya harusi, maana ‘kitchen party’ nyingi zinafanyika mara nyingi siku ya Jumamosi na Jumapili. “Hapo mwanzo nilionekana ni mwanamke mbea na hii niliiona kutoka kwa tabaka wa wanawake wasomi, ila sasa wananielewa na jina kungwi ndilo linanitambulisha kwa kazi yangu.’’ Aidha anakumbana na changamoto ya kushindwa kusaidia vikundi vya wanawake tabala la chini wenye mahitaji ya mitaji ya kuanzisha biashara isiyozidi 500,000. “Wakati mwingine nakosa pesa nawapa mama anakuhakikishia ukimpa laki tano kufanya biashara atainuka na watoto watasoma na kupata mahitaji, wakati mwingine unashindwa umsaidiaje kwa sababu siwezi kusaidia wote, huwa natoa mitaji isiyo na riba walau mara moja kwa mwezi kuanzia 100,000 mpaka 300,000 anasema Irene. Irene pamoja na kutoa ushauri kwa jamii lakini pia amekuwa msaada kwa kina mama ambapo kila mwaka anatoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya kina mama 12 na alianza mwaka 2014. Ni kitukio gani ukikumbuka unacheka? Irene anasema kipindi anamaliza elimu ya sekondari mwaka 1995, mumewe ndio alianza kumfuatilia akimwambia anampenda na anataka amuoe. “Nilisoma Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibosho,mkoani Kilimanjaro, nilipomaliza tu, huyo mume wangu Sebastian alinifuata na kuniambia ananipenda hapo ndio alinitajia na jina lake akasema nimekupenda, nikamuliza kweli? akasema ndio basi si unajua mapenzi ya kujificha ficha, nilikuwa naogopa sana mimba na ukimwi, wazazi wangu walikuwa wakali .

Anasema kuna siku alimfuatilia huyo Sebastian na akamuuliza ,” umesema unanipenda akasema ndio, nikampa kalamu na karatasi nikamwambia andika hapa kuwa unanipenda nijue unamaniisha, akaniuliza niandikeje nikawa namwambia maneno ya kuandika alivyomaliza nikamwambia saini, akasaini basi nikaondoka. Anasema barua ile walikuwa kuisoma wazazi wake na kwamba akiikumbuka huwa anacheka.

Irene anasema hakutumia ujana wake, kwani alipomaliza shule tu, aliolewa, hivyo aliingia kwenye ndoa akiwa na umri mdogo wa miaka 20 ila anamshukuru Mungu mume aliyempata ndiye huyu huyo anayeishi naye hadi sasa zaidi ya miaka 22 ya ndoa.

Ujawahi kukutana na changamoto yoyote kwenye ndoa?

Anasema changamoto zipo maana hakuna binadamu aliyekamilika, kutofautiana kwenye ndao ni vitu vya kawaida, siku za nyuma anasema aliwahi kulia sana, lakini tangu aokoka na kumtegemea Mungu mambo yalibadilika na sasa ndo ni kicheko.

Una mkakati gani kuwasaidia vijana kujitambua? Irene anasema ameanzisha programu maalumu ya kuwasaidia vijana kuanzia miaka 12 hadi 20 waliopo shuleni na anatumia ile kanuni yake ya N-4 ambayo ni najipenda, najithamini, najituma,najitambua inayofundisha vijana mbinu mbalimbali za maisha na kutambua thamani yao hivyo kujitunza ili watimize malengo yao.

Taasisi ya Bembeleza Mbali na kuwa kungwi mfundishaji na mrekebisha jamii, Irene ameanzisha kituo kinachosaidia watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu na hadi sasa kina jumla ya watoto 27 ambao wanahudumia kula,kulala,mavazi na elimu. Anasema kituo hakina wafadhili ila anakiendesha kwa jitihada zake mwenyewe na misaada kutoka kwa wadau wake na watu mbalimbali wanaoguswa ambao hutuma vitu mbalimbali kuwahudumia.

Balozi wa Taulo za kike Irene pamoja na kazi zake amechaguliwa na kampuni inayotengeneza Taulo za Kike ya Sanitary kuwa balozi wake. Anasema kupitia cheo hivho anawasaidia wasichana shuleni kuwapa taulo hizo ili ziwasadia kujihifadhi.

‘’Nazigawa bure taulo hizi na hii inatokana na ukweli kuwa wanafunzi wengi wa kike hususani wale waishio maeneo ya vijijini hapa nchini, wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa vifaa vya kujisitiri wanapokuwa kwenye siku zao. Anasema binti anayekosa vifaa hivyo hata maendeleo yake darasani huwa mabaya hivyo kuna umuhimu wa vifaa hivyo kutolewa bure au kwa gharama ndogo ili kuwasaidia mabinti hayo watimize ndoto zao kielimu. Familia yake Irene ni mke, mama wa watoto watatu, wawili wa kiume wenye umri wa miaka 14 na sita na binti wa miaka 20.

Aidha amefanya kazi ya ujarisiamali wa miaka 20 sasa na shughuli ya ukungwi ameifanya kwa miaka 10 na kwa sasa ni mwanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii akisoma masomo ya maen

JUNI 20 ni Siku ya Wakimbizi Duniani, inayoadhimishwa tarehe kama ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi