loader
Dodoma FC yapania kufanya kweli FDL

Dodoma FC yapania kufanya kweli FDL

UONGOZI wa timu ya soka ya Dodoma Fc umeeleza kuwa kutokana na usajili wa wachezaji ilioufanya katika dirisha dogo itahakikisha inapambana vilivyo katika michuano ya ligi daraja la kwanza (FDL) itakayoendelea kutimua mwishoni mwa wiki hii.

Dodoma ipo kundi B la michuano hiyo na inashika nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 11 na mwishoni mwa wiki hii itashuka kwenye uwanja wake wa nyumbani Jamhuri Dodoma kucheza na Arusha United.

Katika usajili wake wa wachezaji dirisha dogo uliofungwa Desemba 15 timu hiyo imenasa wachezaji wanane katika kukiongezea nguvu kikosi chake.

Kati ya wachezaji hao wanane, sita wamesajiliwa kuitumikia klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja na wawili miaka miwili miwili wataichezea timu hiyo inayonolewa na kocha mkuu Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Waliosajiliwa na timu hiyo ni Adam Siseme aliyetokea Friends Rangers, Peter Mutabuzi aliyetokea Ashanti United, Rajabu Isihaka kutoka Mbeya City, Ahmad Yahya kutoka Toto Africans na Mussa Kirungi kutoka Stand United.

Wengine ni Shabani Kisiga (huru), huku wachezaji wawili Omary Samata na Moshi Mrisho kutoka timu ya vijana ya Dodoma FC wamesaini miaka miwili.

Akizungumza na gazeti hili katibu mkuu wa Dodoma Johnson Fourtnatus alisema kuwa wachezaji waliowasajili na waliowaacha ni kutokana na taarifa ya benchi la ufundi na baadhi ya walioachwa ni kutokana na kucheza chini ya kiwango na wengine ni utovu wa nidhamu.

Wachezaji waliotemwa na timu hiyo ni Salumu Mwinyimadi, Rnock Kubagwa,Juma Mnyasa,Josephat Japhet,Samweli Ngassa na Khatib Jofrey.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2f93dac43b14605b7e9ce3636c6f48b7.jpg

LIVERPOOL inatarajia kutoa jaribio kali kwa ...

foto
Mwandishi: YASINTA AMOS , Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi