loader
Picha

Ali Kiba ashukuru mashabiki kumuamini

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kumuamini na kuthamini kazi anazozitoa na kumpa mwitikio mkubwa.

Kauli hiyo ameitoa juzi baada ya kupokelewa kwa mabango yaliyosomeka ‘mfalme wa Bongo fleva’,kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama Dare es Salaam.

“Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuendelea kusapoti kazi zangu bila kuchoka ni wazi wanakubali kazi ninazoachia na ndio maana zinapata mwitikio mkubwa kwenye matamasha makubwa kama hapa nchini na nje ya nchi,” alisema.

Kiba alipokelewa kwa shangwe katika tamasha hilo hali iliyoonesha kukubali wimbo wake mpya wa Katoto alioutoa wiki iliyopita.

Nyota huyo wa bongo fleva na mchezaji wa timu ya Coastal Union ya Tanga inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara alisema amejipanga kuachia ngoma mfululizo kwa mwaka mpya ili kuendelea kuwapa burudani mashabiki wake.

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya ...

foto
Mwandishi: Tizo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi