loader
Picha

Vijana 20,000 kufunzwa teknolojia ya kitalu nyumba

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa Sh bilioni 2.9 kuwajengea vijana wapatao 20,000 ujuzi kupitia kilimo cha kisasa kutoka halmashauri 84 zilizopo kwenye mikoa 12, kutumia teknolojia ya kitalu nyumba.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde (pichani) alisema hayo juzi katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi huo kwenye Kituo cha Ushirika wa Wahitimu Wajasiriamali wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUGECO).

Mafunzo hayo ya wakufunzi wa mafunzo ya kilimo cha kitalu nyumba yanawashirikisha wataalamu vijana 50 wa nyanza mbalimbali ambao baada ya kumaliza watapelekwa katika halmashauri hizo.

Mavunde alisema lengo la mradi huo kwa mwaka huu wa fedha ni kuwafikia vijana 20,000 kwa maana angalau vijana 100 kutoka kila halmashauri nchini . Aliitaja mikoa hiyo ni Mwanza, Iringa, Ruvuma, Shinyanga, Geita, Mbeya, Lindi, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Kagera na Simiyu katika kipindi cha Januari hadi Machi 2019 na mikoa ilioyosalia kipindi cha Machi hadi Juni, 2019.

Mavunde alisema kwa kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo nchini ambayo ndiyo kimbilio la wananchi walio wengi, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kupitia Ibara ya 6(a), inaelekeza serikali juu ya kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za kisasa na wataalamu wa ugani. Pia kuwapa mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao, ambazo kwa pamoja zinalenga kujenga mazingira mazuri ya kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kiuchumi hasa katika kilimo.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutambua wajibu wake imeandaa programu maalumu ya kuwajengea vijana ujuzi kwenye kilimo cha kisasa na kwa mwaka huu wa fedha, wameanza na utumiaji teknolojia ya kitalu nyumba.

“Mafunzo haya yatafanyika katika mikoa yote Tanzania Bara na katika kila halmashauri,” alisisitiza Mavunde. Alisema kwa kuanzia kila halmashauri itatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati ya hao, 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga vitalu nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hicho, wasikose wataalamu wa kuwajengea vitalu nyumba. Alisema serikali kwa sasa imeelekeza nguvu kuongeza uzalishaji na mnyororo wa thamani katika mazao ya chakula na biashara, kwa kulenga kupunguza na ikiwezekana kuondoa changamoto katika sekta ya kilimo ili iwe na tija.

Alisema katika kuhakikisha inajenga uwezo wa vijana kiuchumi, Ofisi ya Waziri Mkuu ilihamasisha kampuni za vijana kushiriki katika zabuni ya kutoa mafunzo ya kilimo cha kitalu nyumba. Mavunde alisema kampuni tatu za vijana zenye uwezo na uzoefu katika masuala ya kilimo cha kitalu nyumba zilishinda zabuni hiyo, ambazo ni Royal Agriculture Ltd, Holly Agriculture Group Ltd na Ushirika wa Wanafunzi Wajasiriamali Waliohitimu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUGECO).

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO, Revocatus Kimario alisema licha ya juhudi kubwa za kufanya uendelevu wa programu za kutengeneza ajira kwa vijana kupitia kilimo kuwa ya mafanikio makubwa zaidi, bado kuna changamoto nyingi zikiwemo uwezo mdogo wa kifedha wa kuendeleza mawazo bunifu na kukuza teknolojia zinazobuniwa na vijana ili ziwe na matokeo

JESHI la Polisi mkoani Manyara linawashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kumteka ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi