loader
Picha

Pluijm asaka ubingwa Azam FC

KOCHA wa Azam FC, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema nia na lengo lake la kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi ni kuhakikisha wanatetea tena taji hilo na sio jambo jingine.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya Yanga, ambao waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya kikosi cha Yanga kilichosheheni wachezaji chipukizi, alisema kuwa ili kuhakikisha hilo linatimia, ndio maana aliamua kuwachezeshesha wachezaji wake wanaocheza Ligi Kuu Bara.“Nimeshiriki ili niweze kuchukua ubingwa na kutetea taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo na sio jambo jingine, “alisema Pluijm.

Hatahivyo, alisema kuwa ushindi alioupata anaimani kuwa ameifunga Yanga yenyewe bila kujali wachezaji waliochezeshwa.

“ Mimi najua nimecheza na Yanga sasa iwe A au B, ninachojua hii ni Yanga tu,” alisema. Aidha, alisema kuwa timu hiyo pamoja na kuwa wameambiwa ni timu B, lakini imewapa upinzani wa hali ya juu na kuwasifia wachezaji hao kwa kiwango kizuri walichokionesha. “Ni vijana wadogo, lakini wamenipa upinzani wamecheza vizuri, “ alisema.

Kwa upande wake, kocha wa Yanga, Noel Mwandila alisema kuwa pamoja na kufungwa kwenye mchezo huo, lakini bado hajakata tamaa ya kufika hatua ya nusu fainali na kutwaa ubingwa. Alisema kuwa haya ni matokeo ambayo yametokana na makosa waliyofanya wachezaji, lakini ameahidi kuyafanyia kazi na kuhakikisha timu yake inashinda katika mechi zijazo. Alisema kuwa bado hajakata tamaa kutokana na kwamba wana mechi mbili mkononi, ambazo anaamini watafanya vizuri na kusonga mbele.

Katika mchezo huo, timu ya Yanga lilifungwa mabao 3-0 katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali kwa pande zote mbili. Azam kwa mujibu wa ratiba wanashuka dimbani Leo Jumatatu kuanzia saa 10:00 jioni kucheza na KVZ wakati Yanga itacheza na Malindi saa 2:15 usiku na mechi yake ya mwisho atacheza na Jamhuri Januari 9.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemrudishia dhamana ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi