loader
Picha

Maazimio hifadhi mazingira Kigoma yasambazwe nchini

HATUA iliyochukuliwa mwishoni mwa wiki na mawaziri sita kufanya tathmini ya athari ya mazingira ya mkoa wa Kigoma na kisha kutoa maazimio tisa, kunusuru tishio ya uhai wa mazingira bora, inastahili kupongezwa.

Athari zilizobainishwa ni pamoja na kuvamiwa kwa hifadhi za misitu na mapori ya akiba kwa shughuli za kilimo, ufugaji, ukataji miti kwa ajili ya nishati, ujenzi na makazi, huku baadhi ya vijiji vikisajiliwa ndani ya maeneo hayo, ambayo katika hali ya kawaida, hayaruhusiwi kuguswa kisheria kwa lengo la kuwa katika hifadhi endelevu.

Katika kukabiliana na hali hiyo, imeamriwa kutumia muda wa miezi sita kuanzia sasa, ambapo pamoja na mambo mengine ifanyike operesheni ya kuondoa uvamizi wa wakulima, wafugaji na wafanya shughuli zisizo halali kwenye misitu na mapori yaliyohifadhiwa kisheria.

Hakuna ubishi kwamba mkoa wa Kigoma, uko mpakani na nchi jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hivyo unakabiliwa na tatizo la wakimbiz, wanaosabaisha athari mbalimbali za mazingira kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujipatia jnishati.

Kwanza tunapenda kuungana na Watanzania wapenda uhifadhi wa mazingira, kwa kuwapongeza kwa dhati mawaziri wote walioshiriki kwa vitendo, kufanya tathmini hiyo ya uharibifu wa mazingira mkoani Kigoma na kupendekeza mbinu za kuikabilia kwa vitendo kujinusuru.

Lakini, sambamba na pongezi hizo, tunapendekeza tathmini ya uharibifu wa mazingira, ifanyike mikoa yote ili kubaini sababu za uharibifu na wahusika katika uharibifu huo na kisha operesheni kama hiyo ya Kigoma, ifanyike bila kufanya ajizi, kwa sababu matatizo mengine yaliyoanishwa Kigoma, yapo karibu kila mkoa hapa nchini.

Katika hatua hiyo, siyo lazima kuwahusisha mawaziri sita walioshiriki katika kampeni ya Kigoma.

Lakini, inatosha kama kila mkoa utafanya tathmini kama hiyo kupitia viongozi wake wa ngazi za mikoa, wilaya na vijiji ili baada ya hapo nchi yote iwe katika mkakati wa makusudi kukabiliana kwa vitendo uharibifu wa mazingira yetu.

Tathmini iliyofanyika Kigoma na hatua zinazochukuliwa kuokoa mkoa huo na hali hiyo, iwe changamoto kwa watakaofanya tathmini katika mikoa yote, kwa lengo la kuipa kampeni hiyo hadhi ya kitaifa.

Katika hili, tunatoa mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, jamii na mashirika yasiyo ya kiserikali, vingozi wa dini, kimila na wananchi kwa ujumla wake, kushikamana kukabiliana na hali hiyo, ambayo ni tishio la uhai wa taifa letu kimazingira.

Hakuna kisichowezekana. Mawaziri wetu sita, wameanzisha kwa vitendo mkakati huo, nasi tuwaunge mkono pia kwa vitendo.

USAFIRI wa mabasi yaendayo haraka maarufu mabasi ya mwendokasi, umekuwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi