loader
Picha

TFF yapiga ‘biti’ watakaovuruga uchaguzi Yanga

Wakati Mbio za kuziba nafasi za uongozi katika klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), Malangwe Mchungahela ametoa onyo kwa wanachama wa klabu hiyo ambao wanaowatishia wagombea kwenye matawi yao.

Akizungumza leo Jumanne, Malangwe amesema kuwa matawi ni mali ya klabu ya Yanga na siyo mali ya mwanachama, hivyo yeyote atakayefanya fujo wakati wa kampeni, Jeshi la Polisi litamshughulikia ipasavyo.

“Kama hutaki kusikiliza sera za mgombea ni bora ukaondoka na siyo kufanya fujo kuzuia kampeni za mgombea, Jeshi la Polisi lipo makini na litahakikisha wote watakaojaribu kuzuia au kufanya fujo wanadhibitiwa kabla ya kutimiza azma yao,” alisema Mchungahela.

Naye ofisa usalama wa TFF, Caf na Fifa, Inspekta Abdallah Hashim ametangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 13 katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya ...

foto
Mwandishi: By Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi