loader
Picha

Kumekucha Uchaguzi Yanga

WAKATI kampeni za uchaguzi wa Yanga zikianza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ametoa onyo kwa wanachama wa Yanga wanaowatishia wagombea wanaotaka kufanya kampeni katika matawi yao.

Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela alisema matawi ni mali ya klabu ya Yanga na siyo mali ya mwanachama, hivyo yeyote ambaye atafanya fujo kumzuia mgombea kufanya kampeni jeshi la polisi litamshughulikia. “Kama hutaki kusikiliza sera za mgombea ni bora ukaondoka na siyo kufanya fujo kuzuia kampeni za mgombea, Jeshi la Polisi lipo makini na litahakikisha wote watakaojaribu kuzuia au kufanya fujo wanadhibitiwa kabla ya kutimiza azma yao,” alisema Mchungahela.

Pia Mchungahela alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Januari 13 katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam na Ijumaa kamati na wagombea wote watakuwa katika mdahalo utakaofanyika Azam TV. Naye ofisa usalama wa TFF, Caf na Fifa, Inspekta Abdallah Hashim alisema Jeshi la Polisi limejiandaa kuhakikisha kampeni zinafanyika salama na baadaye uchaguzi mkuu unafanikiwa ili Yanga ipate viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Awali, akizungumza Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo alisema aliwataka wanachama kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na wanachama wote wenye kadi wataruhusiwa kupiga kura bila kujali ya kadi ya kitabu au laa. “Wanachama wote wenye kadi bila kujali ya kitabu au hizi mpya wanaruhusiwa kupiga kura, hivyo mtu yeyote asiogope kuja kupiga kura kwani hakuna fujo, Jeshi la Polisi limehimarisha usalama,” alisema Lyimo.

Jumla ya wagombea 16 wanawania nafasi mbalimbali, ambapo nafasi ya uenyejikiti wapo ni Dk Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula na Erick Ninga, Makamu Mwenyekiti ni Yono Kevela, Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota. Wagombea wa nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Shafil Amri, Said Kambi, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka na Athanas Peter Kazige.

Uchaguzi huu ni maalum kuziba nafasi za wagombea waliojiuzulu kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa Juni 11 mwaka 2016. Waliojiuzulu ni aliyekuwa Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wanne, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah. Wajumbe waliobaki katika Kamati ya Utendaji ni wanne tu, ambao ni Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay na Hussein Nyika.

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi