loader
Picha

Kuziona Simba, Js Soura 5,000/-

KLABU ya Simba jana imetangaza maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Js Soaura ya Algeria utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii, ambapo kiingilio cha chini kwenye mchezo huo ni 5,000 kwa mzunguko .

Viingilio vingine kwa viti vya Vip B na C ni Sh 10,000 na kiingilio cha juu kabisa ni 100,000 hii ni platinum na watakao chukua tiketi hizo watakaa kwenye viti vya Vip A na magari yao kuegeshwa kwenye hotel ya Serena na kuchukuliwa na gari maalumu kwenda uwanjani na kurudi Taifa wakiongozwa na Polisi wa Usalama Barabarani. Wakati wa Usafiri huo, watu hao watapatiwa vinywaji na kupatiwa jezi mpya za timu hiyo.

Wapinzani wa Simba, JS Soaura wenyewe wanatarajia kuwasili kesho Januari 10 saa nne usiku tayari kwa mpambano huo kwenye Uwanja wa Taifa. Akizungumza kuelekea kwenye pambano hilo Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara alisema wamefanya maaandalizi makubwa kuwakabili wapinzani wao hao ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwenye mchezo huo wa nyumbani.

“Maandalizi yanaenda vizuri na kikosi cha kwanza kinatarajiwa kuwasili leo kutoka visiwani Zanzibar baada ya kucheza mchezo wa jana dhidi ya Mlandege kwenye michuano ya Mapinduzi Cup, wakati huo kikosi cha pili na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza watabaki chini ya kocha msaidizi Niko Nyagawa akisaidiana na Mussa Mugosi kwa mechi zinazofuata” alisema Alisema wanajua wapinzani wao ni wazuri ndio maana wametinga katika hatua hiyo lakini hawatakubali kupoteza mchezo muhimu kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Manara alisema ili kuhakikisha timu hiyo inapata matokeo amezindua kauli mbiu kuelekea kwenye michezo hiyo inayokwenda kwa jina la ‘ Yes We Can’,wakiwa na imani itatumika vizuri uwanjani kwa kuwapa mashabiki ari na kupata matokeo uwanjani Alisema baada ya kutimiza lengo la kwanza kutinga katika hatua hiyo lengo la pili ni kuhakikisha wanafikisha malengo zaidi ikiwemo kupata pointi tisa katika uwanja wa nyumbani.

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi