loader
Picha

Tuijenge Tanzania yetu kwa pamoja

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imeweka historia katika mambo mengi katika kipindi kifupi cha miaka mitatu.

Mbali na utekelezaji wa miradi mbalimbli inayoendelea hapa nchini tena ya mabilioni kwa fedha za ndani, sasa ni huu ujio wa ndege ambayo ni ya pili mpya aina ya Airbus A 220-300 inayowasili nchini kesho kutokea nchini Canada na kufanya idadi ya ndege mpya zilizonunuliwa na Serikali kufikia sita.

Ndege ambazo tayari zilishawasili nchini ni pamoja na Bombardier Dash 8 Q400 tatu zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132.

Mbali na ndege hizo ambazo kwazo zimeweka historia hasa ikizingatiwa kwamba Airbus A220-300 ni toleo jipya kabisa huku Tanzania ikiwa ya kwanza barani Afrika kuziagiza, tayari miradi mikubwa ya umeme na mawasiliano ikiwemo treni ya kisasa ikiwa imeshika kasi.

Mfano ni mradi wa Tanzania Standard Gauge Railway (SGR) ambapo kilometea zipatazo 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro zinaendelea kujengwa kwa kasi huku waandisi wa Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki na Mota-Engil ya nchini Ureno wakishirikiana na wazawa wakifanya kazi usiku na mchana.

Mradi huu haushii hapo, unaendelea hadi Dodoma na baadaye Mwanza na Isaka na Mungu bariki, uko mbeleni mradi huo utaziunganisha Tanzania na Rwanda kupitia Isaka – Kigali Haya ni mafanikio makubwa ya kiuchumi ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imefanya.

Wakati kesho ndege ya sita ikipokelewa, kuna kila haja Watanzania kuwa pamoja ili kumsaidia Rais Magufuli na wetendaji wake aweze kufikia malengo yake.

Nchi zilizoendelea hazikufanya maendeleo hayo kwa siku moja, ndio maana tunasema ni vema kupongezana kwa kila hatua moja huku tukiungana kuwezesha hatu nyingine inayofuata. Ili kuwezesha malengo ya Rais Magufuli kutimia, ni wananchi kulipa kodi, tena kwa usahihi na wakati.

Kukwepa kodi au kufanya udanganyifu wowote katika ulipaji kodi ni kukwamisha juhudu za serikali katika kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kutoka umasikini uliokithiri na kuwa nchi zinazoheshimika.

Tunasema inawezekana kwa sababu kama nchi inaagiza ndege za kisasa ambazo ni za kwanza barani Afrika, ni ukweli ulio wazi kwamba nchi hii si muda mrefu itapokea mataifa mbalimbali kuja kujifunza jinsi ya kufanya mageuzi ya kiuchumi kwa muda mfupi kwa kutumia rasilimali za ndani ya nchi.

Ni kutokana na ukweli huo, kila Mtanzania ajione ni sehemu ya mafanikio haya ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii, kuacha ubabaishaji, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi, rushwa na mengineyo kama hayo ambayo kwayo yamekuwa ndiyo yaliyotufikisha hapa.

Tanzania mpya inawezeka, kila mmoja akifanya kazi yake na akaifanya barabara.

USAFIRI wa mabasi yaendayo haraka maarufu mabasi ya mwendokasi, umekuwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi