loader
Picha

Simba yaisubiri Js Soaura

KIKOSI cha timu ya Simba tayari kimeondoka visiwani hapa na kurudi jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Js Soaura ya Algeria utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Kikosi hicho ambacho kilikuwa kikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi kimeondoka na wachezaji 18 kwa boti ya saa 3:30 asubuhi. Wakati ikiondoka na kukiacha kikosi B cha timu hiyo, tayari Simba ilishatinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo wakati watani zao Yanga walitolewa katika hatua ya makundi. Meneja wa timu hiyo, Abass Ali aliambia gazeti hili kwamba wachezaji hao wameondoka na kikosi B kitabaki kumalizia mechi zilizobaki na wametamba kutwaa taji hilo.

Alisema kuwa baadhi ya wachezaji wazoefu hawakuwemo kwenye kikosi kilichoondoka ili kukiongezea nguvu kikosi hicho cha B, ambacho kiko chini ya kocha Niko Kiondo na msaidizi wake, Mussa Hassan Mgosi. Alisema kuwa kikosi hicho kilichoondoka ndicho kitakachocheza mchezo huo na kuwaomba kuungwa mkono ili waweze kufanya vizuri katika mechi zilizobaki.

“Mchezo wa mwanzo ni vizuri kushinda uwe nyumbani au ugenini tunaomba Watanzania watuombee ili tuweze kuanza vizuri katika hatua hiyo ya makundi, “alisema. Abass alisema kuwa kikosi B kitakachokuwepo kuendeleza mashindano hayo sio kibaya hasa ukiangalia kwamba wengi wa wachezaji, ambao wapo Simba ya Wakubwa nao walitoka huko huko B, Wachezaji waliondoka jana ni John Bocco, Aishi Manula, Shiza Kichuya, Meddie Kagere, Nicholas Gyan, Pascal Wawa, Clatious Chama, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, James Kiote, Deogratius Munish, Hassan Dilunga, Juuko Murshid, Rashid Juma, Mohammed Hussen, Mzamiru Yaasin, Said Ndemla, na Jonas Mkude Wachezaji waliobakia ni , Asante Kwasy, Yusuf Mlipili, Adam Salamba, Ally Salim, Zaana Coulibaly, Abdul Seleman na Mohamed (MO).

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi