loader
Picha

Kocha Aussems amlilia Nyoni

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema ni bahati mbaya kumkosa mlinzi wake, Erasto Nyoni kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya JS Souara unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kurejea Dar es Salaam jana, Aussems alisema ni pigo kumkosa kiraka huyo, ambaye aliumia goti la kulia kwenye mchezo wa Mapinduzi Cup dhidi ya KMKM, lakini anao wachezaji wa kutosha hivyo mashabiki wasiwe na hofu. “Ni bahati mbaya Erasto Nyoni atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tano, ndivyo mchezo wa soka ulivyo unaweza kumhitaji mchezaji muhimu kwenye mchezo muhimu lakini ukamkosa,” alisema Aussems.

Pia amekiri kuwa atafanyia kazi pengo hilo kwa kuwatumia wachezaji wengine kwenye kikosi chake na tayari ameshawaandaa kwa ajili hiyo kuanzia mchezo wa juzi dhidi ya Mlandege ambao walishinda kwa bao 1-0. Aidha, alisema anaamini klabu yake itaifunga JS Souara katika mchezo wa Jumamosi na kufanya vizuri katika mechi zingine hadi kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

“Naamini Jumamosi tutashinda kwani mashabiki wanatoa mchango mkubwa, hivyo hatutawaaangusha ili tufuzu robo fainali na baadaye fainali hata kama tuko na timu ambazo zilicheza fainali msimu uliopita,” alisema Aussems Simba ipo kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo DRC na JS Saoura ya Algeria na Al Ahly ilicheza fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Esperance Tunis ya Tunisia ambapo Esperance ilishinda ubingwa kwa uwiano wa mabao 4-3 huku AS Vita Club ikicheza fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco. Simba imerejea jana kutoka Zanzibar katika kombe la Mapinduzi baada ya kufuzu nusu na kuwaacha wachezaji wa kikosi cha pili, ambao wataendelea na mashindano hayo.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi