loader
Picha

Mabalozi 50 kuhudhuria sherehe za mapinduzi

JUMLA ya mabalozi 50 wanaoziwakilisha nchi zao nchini pamoja na viongozi wa mashirika ya kimataifa na taasisi za fedha wanatarajiwa kuhudhuria katika sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zitakazofanyika Pemba, kesho kutwa.

Akizungumza na baadhi ya mabalozi wadogo waliopo Zanzibar, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ya Zanzibar, Mohamed Haji Hamza ameisema maandalizi ya ujio wa mabalozi hao kwa ajili ya safari ya Pemba yamekamilika.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imejipanga kuona kwamba sherehe hizo zinafanikiwa na kuhudhuriwa na viongozi wenye hadhi ya kibalozi.

Hamza alisema usafiri wa mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa umeandaliwa kuanzia Tanzania Bara hadi watakapofika Zanzibar na tayari kwa safari ya Pemba.

Aidha alisema wapo mabalozi watakaofunga safari moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Pemba na kurudi ambapo usafiri umetayarishwa.

“Maandalizi ya safari ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar yamekamilika ambapo tunatarajia jumla ya mabalozi 50 pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa na taasisi za fedha watafunga safari kwenda Pemba,” alisema.

Alisema hiyo ni moja ya fursa kubwa ya mabalozi kuona mandhari ya kisiwa cha Pemba ambao wapo watakaopata nafasi ya kutembelea baadhi ya vivuto vya utalii.

Mapema Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Abdallah Hassan Mitawi aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria sherehe hizo ambazo ni matokeo ya wananchi wa Zanzibar kufanya Mapinduzi yaliyoung'oa utawala wa Kisultani na wazalendo walio wengi kushika hatamu ya madaraka.

Amesema ni miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo mafanikio makubwa yamefikiwa ikiwemo ya kiuchumi, sekta ya elimu na afya pamoja na mawasiliano ya miundo mbinu.

“Wananchi wa Zanzibar wanayo kila sababu ya kusherehekea miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo ndiyo yaliyowaweka madarakani wananchi.”amesema.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi