loader
Picha

Watumishi wa Ardhi wasakwa viwanja 9,000

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeanza operesheni maalum kubaini wamiliki hewa wa viwanja zaidi ya 9,000, vilivyoandikishwa kumilikiwa na watumishi wa wizara hiyo kwa njia isiyokuwa halali.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ilibainisha kuwepo kwa idadi kubwa ya viwanja, vinavyomilikiwa na wafanyakazi hao kwa majina bandia au anuani za uongo. Alisema watumishi hao wamejimilikisha isivyo halali ili waje kuviuza kwa wananchi kwa njia za udanganyifu na kuwa wapo watumishi, ambao wamepima viwanja vya wananchi mara mbili mbili na kuwasababishia kero wananchi hao. Aliongeza kuwa idadi kubwa ya viwanja hivyo havijalipiwa kodi na pia havijaendelezwa kwa kuwa vimeachwa kwa muda mrefu bila ya shughuli za kibinadamu kufanyika hali inayowaathiri wakazi wengine wa maeneo hayo.

Alisema,“wizara imejipanga kunasa viwanja vyote ambavyo umiliki wake una mashaka na vitachukuliwa na kurejeshwa serikalini hivyo basi wananchi mnaombwa kutoa ushirikiano stahiki ili operesheni hii iwe na tija.” Akizungumzia kuhusu athari zaidi za kutoendelezwa kwa viwanja hivyo, alisema kuwa ni sawa na kuwadhurumu haki wananchi wengine kumiliki ardhi na kuongeza kuwa kwa kutokuendelezwa huko, kunasababisha uwepo wa nyoka, uchafu au hata uharifu kwa wananchi waishio maeneo husika au jirani.

Aliwataka wananchi waishio jirani na maeneo yasiyoendelezwa kwa zaidi ya miaka 10 bila ya kuwaona wamiliki wake kutoa taarifa ili yaanze kuchunguzwa. Kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni, viwanja hivyo na idadi yake ni Mbweni Mpiji viwanja 3,544, Mbweni JKT viwanja 1,424, Mivumoni viwanja 1,508 na Bunju viwanja 4,868. Kwa upande wa Temeke ni maeneo ya Tuangoma yenye viwanja 3,384 na Kizota ikiwa na viwanja 2,362.

Kwa upande wa Wilaya ya Kigamboni, maeneo yenye viwanja vya aina hiyo ni Mtoni Kijichi, viwanja 1,776, Mwongozo viwanja 2,754 na Vijibweni viwanja 38. Maeneo mengine ni Kibada viwanja 6,223 na Gezaulole viwanja 1,128, wakati Wilaya ya Ilala eneo la Buyuni Chanika viwanja 7,570 na Mwanagati viwanja 2,164. Waziri Lukuvi aliwataka watu wenye taarifa za watu wanaomiliki viwanja visivyoendelezwa kwa muda mrefu kwenye maeneo hayo, kumpigia simu yake ya mkononi namba 0755 333334 huku akiwahakikishia usalama wao kuwa hawatajulikana kuwa ndio wametoa taarifa hizo.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi