loader
Picha

PSSSF waanza kuhakiki wastaafu

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa PSSSF, umeanza kufanya uhakiki wa wastaafu na wategemezi wa mfuko huo kuanzia sasa hadi mwezi Machi, mwaka huu Tanzania Bara na Visiwani.

Ili kuweza kufanikisha kazi hiyo, uongozi wa mfuko huo umetaja vigezo vitakavyotumika ili kutambua uhalali wa wastaafu hao, ambapo wahusika wametakiwa kufika katika ofisi za mfuko huo wakiwa na picha moja ya pasipoti, kitambulisho cha Taifa au cha mpiga kura na nakala ya kadi ya benki. Kwa mujibu wa taarifa ya PSSSF iliyotolewa kwa umma jana, wahusika wanaotakiwa kufuata masharti hayo ya uhakiki ni waliokuwa wanachama wa mifuko ya LAPF, GEPF, PSPF na PPF ambapo awali ilikuwa ni mifuko inayojitegemea.

Kutokana na kuunganishwa kwa mifuko hiyo, sasa imezaliwa mifuko miwili ambayo ni wa PSSSF unaohusika na watumishi wa umma na Mfuko wa NSSF unaoshughulikia watumishi walio wa sekta binafsi. Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Rais John Magufuli, kuagiza mifuko hiyo kuanza kulipa mafao kwa kutumia mifumo iliyokuwa inatumiwa na mifuko kabla ya kuunganishwa.

Alitoa agizo hilo alipokutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Desemba 28, Ikulu jijini Dar es Salaam. Katika maagizo hayo, Rais Magufuli pia aliagiza wafanyakazi waliokuwa kwenye ajira za muda zisizokuwa za kitaaluma, kulipwa mafao yao yote, pindi tu mradi husika unapomalizika au wakisitishiwa mkataba wao. Hatua hiyo ya Rais Magufuli iliibua shangwe kutoka kwa wafanyakazi na wastaafu na kufuatiwa na maandamano, yaliyofanyika katika miji ya Dar es Salaam na Dodoma ili kuunga mkono agizo hilo.

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha ...

foto
Mwandishi: Evance Ngingo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi