loader
Picha

Ummy ampokea kwa bashasha Dk Chaula

KWA kuzingatia kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali hawaelewani na wanalumbana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemkaribisha kwa bashasha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Zainabu Chaula.

Dk Chaula kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Katibu huyo mkuu mpya anachukua nafasi ya Dk Mpoki Ulisubisya, ambaye ameteuliwa na Rais kuwa balozi. Katika hotuba yake kwa taifa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Dk Chaula, Rais Magufuli alionesha kukerwa na baadhi ya viongozi kulumbana na kutumiana ujumbe wa simu na wengine kufikia hatua ya kutukanana. Miongoni mwa viongozi aliowataja kuwa hawaelewani na walikuwa wakitumiana ujumbe wa simu ni Waziri Ummy na Katibu wake mpya, Dk Chaula.

Kutokana na viongozi hao wawili ambao Rais Magufuli alisema kuwa wote wanatoka mkoani Tanga kulumbana, ameamua kumteua Dk Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ili wakae pamoja na kama ni kulumbana, basi walumbane vizuri. Kwa kuonesha kutii kauli ya Rais, Waziri Ummy kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameoneka kumpokea Dk Chaula kwa tabasamu na kumtaka washirikiane katika kuendeleza juhudi za kuboresha huduma za afya nchini.

Mbali na kumpokea Dk Chaula, Ummy pia kupitia ukurasa wake huo wa Twitter, alimshukuru Dk Ulisubisya kwa ushirikiano mkubwa aliompatia katika kusimamia sekta ya afya nchini na kumtakia kila heri katika majukumu yake mapya. Pamoja na malumbano yao, Rais Magufuli aliwapongeza Waziri Ummy na Dk Chaula kwa kufanya kazi nzuri katika sekta ya afya. Viongozi wengine aliowataja kulumbana ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo na Mbunge wa Jimbo hilo, huku akisema kuwa malumbano yaliyokuwepo kati ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Mkuu wa Wilaya, yamekwisha baada ya yeye Rais kuwatumia ujumbe maalumu.

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi