loader
Picha

Pacha wa Kagera watengenezewa miguu bandia

WATOTO mapacha wa Elmenesia na Anisia Benatus, wanaendelea vema na tayari wametengenezewa miguu ya bandia. Pacha hao wapo kwenye matibabu nchini Israel, baada ya kutenganishwa, na kila mmoja amebaki na mguu mmoja.

Hatua hiyo imewafanya madaktari wa Hospitali ya Riyadhi (pichani) ambao waliwatenganisha, kuwatengenezea miguu ya bandia. Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette. com, pacha hao wanaendelea vizuri na wapo chini ya uangalizi maalum hadi hapo hali zao zitakapotengemaa sawa sawa. Pacha hao walitenganishwa na jopo la wadaktari 32 kwa muda wa saa 13 Desemba 23 mwaka jana.

Upasuaji huo uliofanyika katika Hospitali ya Mfalme Abdullah (King Abdullah Children’s Specialist Hospital), iliyopo mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.

Watoto hao, Almenesia na Anesia walizaliwa Januari 29, wilayani Misenyi mkoani Kagera katika Kituo cha Masista cha St Theresa Omukajunguti Kata ya Kyaka na kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam mwezi Februari mwaka jana. Watoto hao walikuwa wameungana eneo kubwa la kifuani na tumbo, lakini kila mmoja ana mfumo wake wa hewa.

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi