loader
Picha

NEMC yawakaba koo wataalam wa mazingira

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limetoa miezi miwili kwa wataalam na makampuni ya ushauri wa mazingira nchini, kulipa ada zao za mwaka kwa huduma hizo, kama ilivyopangwa kinyume na hapo hatua za kisheria zitafuata ikiwa pamoja na kuwafutia leseni za kutoa huduma husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alisema ada hizo za mwaka zipo kwa mujibu wa sheria na kuwataka watalaamu kulipa kwa wakati ili kufanikisha shughuli za uboreshaji sekta mazingira ikiwemo kutoa ushauri pamoja na ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali ya mradi.

‘’Mara baada ya muda huo kupita baraza litafanya ukaguzi maeneo yote nchi nzima na endapo itabainika wadau hao hawajalipa ada stahiki, basi Baraza litafuta leseni zote na nakuwachukulia hatua za kisheria dhidi ya wadaiwa sugu,”alisema Dk Gwamaka. Alieleza ada hizo zitumika kuboresha utoaji wa huduma na pia husaidia katika kuandaa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira. “Baraza limeweka utaratibu maalumu wa kukagua madeni na utendaji kazi wa mataalamu wa mazingira ili kujiridhisha utendaji kazi wao na kuhakikisha kama kazi wanazofanya zina weledi ambao utasaidia kuboresha mazingira,” alisema.

Dk Gwamaka alisema NEMC ni taasisi mtambuka ambayo ipo mstari wa mbele kuchagiza maendeleo ya uchumi na viwanda hapa nchini kwa kuhakikisha wanatoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira kwa wawekezaji wote. ‘’Niwaombe watu wote ambao wana vyeti vya tathmini ya athari kwa mazingira, wataalamu na makampuni ya ushauri ya mazingira kufuata sheria na kanuni za mazingira ili kuepuka usumbufu katika utendaji kazi,” alisema Dk Gwamaka.

Alieleza Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 inamtaka mwenye mradi kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kwa mradi anaosimamia au kufanya ukaguzi wa mazingira ili aweze kupata cheti cha mazingira ambacho kinatolewa na NEMC pekee nchi nzima.‘

’Kama huna cheti baraza litakutaka usajili mradi wako kwa kutembelea ofisi zetu zilizoko Mikoa ya Dar e s salaam, Arusha, Dodoma, nyanda za juu ofisi zipo Mbeya, Mtwara na Mwanza ili kuwa katika mazingira mazuri yakuendelea mradi wako,” alisema Dk Gwamaka Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki, Jaffari Chimgege alisema timu yake imejipanga kikamilifu kutembelea kanda yake inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam , Tanga Morogoro na Pwani ili kujiridhisha kama masharti ya cheti yametekelezwa.

‘’Ni mategemeo yetu kama baraza kila mtu ambaye anacheti cha mazingira atakuwa ametekeleza vizuri masharti ya cheti, ikiwemo kulipia ada ya mwaka,’’ alisema Chimgege. Katika hatua nyingine, Chimgege alieleza kuwa NEMC imesajili wataalamu elekezi zaidi ya 1,000 na makampuni ya wataalamu elekezi zaidi ya 200, lengo likiwa ni kurahisisha huduma zinazotolewa na baraza hilo nchi nzima. ‘’Kama Baraza, tumejipanga kuhakikisha hatupati mkwamo kwa namna yoyote ile kwani tumeshasajili wataalamu elekezi zaidi ya 1,000 na makampuni ya wataalamu elekezi zaidi ya 200 kwa lengo la kurahisisha huduma nchini,” alisema Chimgege.

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi