loader
Picha

Aitaka TBC kutekeleza kikamilifu majukumu yake

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi amesema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), lina wajibu mkubwa kwa Watanzania kuhakikisha wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali.

Aidha upatikanaji wa huduma bora pamoja na kuuhabarisha umma kuhusu fursa zilizopo za maendeleo, hivyo TBC ina wajibu wa kufika maeneo yote ya nchi hata pale ambapo vyombo vingine vya utangazaji vipo. Mlawi alisema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la TBC, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam. Alisema mkazo wa Serikali ya Awamu ya Tano ni Uchumi wa Viwanda, hivyo shirika hilo kama chombo cha umma cha utangazaji, kina jukumu kubwa la kuwezesha azma hiyo kufikiwa kwa kuelimisha kupitia vipindi vinavyohamasisha uwekezaji na uanzishaji wa viwanda vitakavyoongeza ajira, kuongeza thamani ya mazao na hivyo kuongeza mapato.

Alisema kwa kuelewa umuhimu wa shirika hilo, serikali imetoa kipaumbele ili itekeleze majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti ya maendeleo ya shirika kutoka Sh. bilioni moja mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh. bilioni tano mwaka 2018/19. “Hatua hiyo imeimarisha usikivu wa Redio TBC Taifa na TBC FM katika maeneo mbalimbali nchini hususan ya mipakani, mifumo ya urushaji matangazo kwa njia ya kidigitali imeboreshwa, mitambo mipya ya kupooza katika studio imefunga pamoja na kununuliwa kwa magari tisa kwa ajili ya shughuli za utangazaji,” alisema. Pia alisema bajeti ya matumizi mengineyo imeongezeka kutoka Sh. milioni 400 mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh. bilioni 4.5 mwaka 2018/19, ambayo ni kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa shirika.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi