loader
Picha

Tanesco yajenga mtambo wa umeme megawati 400

SHIRIKA la Umeme (Tanesco) linajenga mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 400 ambao utatosheleza mahitaji ya nishati hiyo katika jiji la Dodoma.

Akikagua mtambo huo unaojengwa katika eneo la Zuzu, nje kidogo ya jiji la Dodoma, Waziri wa Nishati, Dk Merdard Kalemani alimtaka mkandarasi kukamilisha ya ujenzi ndani ya muda wa mkataba unaoishia Januari 28, mwaka ujao. Waziri Kalemani alisema mtambo huo ni muhimu kutokana na jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi, hivyo mahitaji ya umeme ni makubwa kwa serikali na wakazi wa jiji hilo. “Kukamilika kwa mtambo huo kutalifanya jiji la Dodoma kuwa na umeme wa uhakika wakati wote,” alisema.

Kuhusu hali ya kukatika umeme jijini humo, Dk Kalemani aliwataka Tanesco siku 14 tangu Januari 09, mwaka huu, kuhakikisha tatizo la kukatika katika kwa umeme linakomeshwa mkoani humo. Dk Kalemani alisema Tanesco wanatakiwa kuhakikisha umeme unapatikana kwa uhakika na wakati wote, hivyo wana wajibu wa kuweka vifaa muhimu katika vituo vidogo vya umeme vyo mkoani kupata umeme wa uhakika.

Alisema Tanesco inatakiwa kupeleka kwenye stoo za vifaa muhimu katika vituo vidogo vya umeme mkoani kudhibiti hali ya kukatika umeme ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara mkoani. “Katika muda wa siku 14 sipendi kuona upande wowote wa jiji la Dodoma umeme umekatika baada ya kupeleka vifaa vya kudhibiti hali hiyo katika vituo vidogo vya umeme mkoani,” alisema.

Mkoa wa Dodoma unazalisha umeme wa megawati 48 huku mahitaji yake halisi ni megawati 18. Akizungumza, Meneja wa Tanesco mkoani hapa, Zakayo Themu alisema wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha kwamba tatizo la kukatika katika umeme linapungua na kuisha kabisa mkoani Dodoma.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi