loader
Picha

Wakazi Chilonwa waomba majisafi, salama

WANANCHI wa Kijiji cha Mahama, Kata ya Chilonwa wilayani Chamwino wameiomba serikali kuwapatia majisafi na salama kutokana na kuchoka kutumia maji ya kwenye makorongo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi, wananchi hao walisema serikali isaidie ili wapate huduma ya maji ili waachane na maji ya kwenye makorongo ambayo si safi na salama. Mmoja wa wananchi hao, Lameck Mkavu alisema Chilonwa ambayo ni makao makuu ya kata haina maji kwa kipindi kirefu.

“ Vijana zaidi ya 50 tuliungana na kwenda ofisi ya diwani ili tujue hatma ya ukosefu wa maji kwani awali tuliambiwa kuna mradi mkubwa wa maji, haukuja hata mabomba yaliyoletwa kutandazwa yakaondolewa kutokana na kwamba ni mabovu,” alisema. “Kila tunapoenda kwa diwani tunapewa majibu yasiyoridhisha. Waswahili husema, mwenye kiherehere huwa hapewi pole’ lakini tunaamini kwamba serikali itasikia kilio hiki na kutusaidia,’” alisema.

“Hapa tuliambiwa tutaletewa mradi wa maji walikuja hata kuchimba mtaro lakini mwisho wa siku wale watu hawakuonekana, mabomba yakaondolewa, yale machache yaliyoachwa yalipigwa na jua yakapasuka,” alisema “Tunajiuliza fedha za mradi ule zilikwenda wapi kwani tunasikia fedha za mradi huo zilishatolewa lakini wananchi wanataabika na ukosefu wa maji,” alisema.

Alisema sasa wanatumia maji kutoka kwenye makorongo ambako wamekuwa wakichimba visima na mvua ikinyesha huwa vinafukiwa. “Wakati wa mvua upatikanaji wa maji unakuwa mgumu wafugaji wengi huwa wanachungia milimani na hujisaidia huko sasa wakati wa mvua maji yenye vinyesi hushushwa na maji hadi kwenye makorongo tunayochotea maji na watu hutumia maji hayo kwa matumizi ya nyumbani jambo ambalo ni hatari kwa afya,” alisema.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi