loader
Picha

RC aagiza wasio na sare kwenda sekondari

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wazazi na walezi wilayani Karatu kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule hata kama hawana sare za shule.

Aidha ameagiza uongozi wa serikali ya kijiji cha Lositete kuchukuliwa maelezo na polisi kuhusu sababu za kutochangia maendeleo ya elimu, badala yake wanaingiza siasa na kusababisha saruji kuganda.

Gambo alitoa agizo hilo jana katika kijiji cha Lositete, kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu alipokwenda kukagua hali halisi ya madarasa pamoja na idadi ya wanafunzi walioanza masomo ya kidato cha kwanza.

Alitoa agizo hilo jana kutokana na taarifa ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Upper Kitete, Josephat Mau iliyodai kuwa wanafunzi tisa kati ya 171 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni hapo wameripoti shule. Mwalimu Mau alisema wanafunzi hao 162 hawajaripoti shuleni hapo kutokana na kukosekana na sare za shule huku walioripoti wakiwa ni tisa kwa sababu ya wazazi au walezi wao kutouza maharage kwani hakuna soko.

Baada ya mwalimu huyo kutoa taarifa hiyo, Gambo aliagiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kuripoti shuleni na nguo za nyumbani hata kama hawana sare ili waendelee na masomo wakati wazazi wao wakisubiri kuwanunnulia mahitaji ya shule. “Rais ameagiza elimu bure hivyo wazazi au walezi watoeni watoto wenu majumbani ili waende shule bila ya kuwa na sare za shule huku mkiendelea kutafuta sare lakini pia nasisitiza nyie wananchi acheni kuingiza siasa kwenye masuala ya maendeleo, “alisema.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete, Gambo aliagiza mwenyekiti wa kijiji cha Upper Kitete, William Safari pamoja kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ya kijiji ambayo wananchi wanadai hawajasomewa tangu mwaka 2017 hadi mwaka jana. Awali, baadhi ya wananchi walidai kuwa wameshindwa kujenga madarasa pamoja na maabara kwa sababu walichanga fedha ambazo inadaiwa zililiwa na aliyekuwa mkuu wa shule hiyo, Andrew Sulle. Anadaiwa kuchukua Sh milioni nane.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo alisema wananchi zaidi wa vijiji vya Lositete na Upper Kitete wanapenda kuingiza masuala ya siasa katika maendeleo. Alisema amejitahidi kutatua changamoto zao ikiwamo kuhakikisha mwalimu huyo anachukuliwa hatua za kinidhamu na ameshahukumiwa kifungo. Alisema wanafunzi 5,313 walifanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana huku wanafunzi 4,000 sawa na asilimia 75.3 walifaulu.

Wanafunzi 3,446 wamepangwa kwenye shule za kata zilizokuwa na madarasa 83 na wanafunzi 539 walikosa nafasi. Alisisitiza kuwa wanafunzi hao 539 waliokosa nafasi hivi sasa wameshaanza masomo katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kutokana na kubainika kuwapo shule ambazo wanafunzi hawakupangwa. Alisema wanaandika barua kwa wadau na kuhamasisha wanananchi kujenga madarasa pamoja na kukarabati viti na meza ili wanafunzi waweze kusoma.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Karatu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi